
Wabunge wa Uganda walipiga kura kutaka kujiongeza mishahara na marupurupu
Kumezuka malalamiko nchini Uganda baada ya wabunge kununuliwa tabiti au (iPads) kwa pesa za Umma.
Afisaa mkuu wa Bunge amesema kuwa tabiti hizo zitawafanya wabunge kuwa makini wakati wa vikao vya bunge.
Pia
alisema kuwa pesa walizonunulia iPad hizo zitasaidia kuepuka kutumia
kiwango kikubwa cha karatasi na kupunguza gharama ya matumizi.Kamishna
wa bunge Emmanuel Dombo amesema kuwa wabunge sasa wanaweza kupata
stakabadhi zao rasmi wakati hata wakiwa nje ya ofisi zao au wakiwa
safarini.
Wabunge wote wa bunge la Uganda ambao idadi yao ni 375, wanunuliwa zilizogharimu kima cha dola laki tatu na sabini.

Wakosoaji
wanahoji ikiwa wanasiasa wanajua hata kuzitumia tabiti hizo na kusema
kuwa tayari wananchi wanalipa pesa nyingi sana kwa mishahara ya wabunge
Mwaka jana wabunge wa Uganda walipiga kura kutaka mishahara na marupurupu yao kuongezwa kwa asilimia arobaini.
Pia walipokea marupurupu ya zaidi ya dola 40,000 ili kujinunulia gari jipya.
Mbunge wa Uganda kwa sasa hulipwa, dola elfu nane , ingawa nchi hiyo inakumbwa na matatizo ya kiuchumi.
Wananchi
wanasema kua hatua hii ya serikali ni kuharibu pesa za mlipa kodi,
ikizingatiwa kuwa wabunge hao wanalipwa mishahara ya juu ambayo
inawawezesha kujinunulia vifaa hivyo wao wenyewe.


No comments:
Post a Comment