Takriban wanajeshi watano na afisa wa jeshi wameuawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu,nchini Somalia mashuhuda wameeleza.
Mlipuko huo unaelezwa kutokea wakati wanajeshi hao wakipata malipo yao nje kidogo ya mji huo.
Sababu ya mlipuko huo haijafahamika,majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.
Wanamgambo
wa kiislamu, al Shabab walitimuliwa kwa nguvu mjini Mogadishu mwaka
2011 lakini wameendelea kufanya mashambulizi nchini humo
Kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la al -Qaeda linadhibiti maeneo kadhaa katikati ya Somalia.
No comments:
Post a Comment