Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, December 13, 2013

Zitto hana majina ya watu walioficha mabilioni ya fedha Uswisi??


 
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema  (pichani kulia) amesema

wanashughulikia kisheria suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe  (pichani chini) kudanganya bunge na kamati kuhusu majina ya watu walioficha mabilioni ya fedha Uswisi. 
Jaji Werema, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya kuchunguza
madai ya mabilioni hayo amesema ili kumalizia uchunguzi wa fedha hizo ameomba Naibu Spika wa bunge kuongezea kamati hiyo miezi sita. 
Akitoa majumuisho ya taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati
ya Bunge ya Katiba ,sheria na Utawala , Jaji Werema alisema alishangaa kitendo cha Mhe. Zitto kutaka suala hilo liangalie mfumo na siyo majina ya watu walioficha mabilioni hayo. 
Jaji Werema alisema awali yeye alishauri kuangalia mfumo wa uwekaji wa
fedha hizo lakini Mhe. Zitto alikataa na kusema anataka kutoa dukuduku kwa kutaja majina ya watu walioficha hizo. 
Alisema mwezi Februari kamati ilikutana na Mhe. Zitto na kuwaeleza
kuwa ana taarifa na nyaraka na kutoa masharti lakini aliondoka ka kwenda katika kambi ya jeshi kwa mafunzo ambako kamati ilimfuata lakini bado aliwataka kukutana Dar.
Alisema Mei mwaka huu amekuwa akiichenga kamati hiyo hadi Oktoba ndipo alipokiri kwa kiapo maalum kuwa hakuwa na jina wala
akaunti ya mtu yeyote ambaye ana fedha nchini Uswizi. 
“Jambo la kushangaza ni leo kudai serikali haina dhamira na
suala la walioficha fedha uswis?kwa kweli  Mhe. Zitto Kabwe ni mzigo na sasa tunaingia kufanya kazi hiyo ya uchunguzi kama serikali kwa kutafuta taarifa bila kumuonea mtu”alisema  Jaji Werema .

No comments:

Post a Comment