Bunda. Polisi Wilaya ya Bunda, wanamshikilia baba mwenye umri wa miaka 54 kwa tuhuma kuoa mwanafunzi wa kike wa umri wa miaka minane.
Msimamizi wa Dawati la Jinsia katika
Kituo Kikuu cha Polisi Bunda, Rita Charles alisema baba huyo mkazi wa
Kijiji cha Nyaburundu wilayani Bunda alikamatwa jana akiwa anaishi na
binti huyo (jina limehifadhiwa) kama mke wa nyumbani baada ya kutoa
kishika uchumba kiasi cha Sh55,000 kwa wazazi wake.
Ilielezwa kuwa mwanaume huyo kabla ya
kumwoa mtoto huyo aliyekuwa anasoma darasa la kwanza katika Shule ya
Msingi Nyaburundu, alimchumbia kwa wazazi wake na kutakiwa atoe ng’ombe
watano za mahari ndipo akatoa kishika uchumba hicho na mtoto huyo
kuondolewa shule. “Tulifanikiwa kumkamata mwanamume huyo baada ya kupata
taarifa kutoka kwa wasamaria wema,” alisema Rita.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Alisema siku ya Mwaka Mpya, alichukuliwa na dada yake na kumpeleka kwa mume wake huyo ili aanze maisha ya ndoa.
Hata hivyo, alisema alipofika, usiku huo
walilala kitanda kimoja wote watatu (baba muoaji, muolewaji na dada wa
muolewaji) na kwamba mwanamume huyo alianza kufanya mapenzi na dada yake
na baadaye akamgeukia ‘mkewe’ kuanza kumnyonya maziwa.
“Tulilala wote watatu na alifanya mapenzi na dada yangu, mimi akininyonya maziwa,” alisema mtoto.
MWANANCHI
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment