Wananchi wakiwa katika mkutano huo leo.TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI(USIPITWEEEEEEEEEE) |
Wananchi Iringa mjini wakiwa wamejipanga kwa maswali katika mkutano wa CCM Iringa mjini leo |
Diwani wa kata ya Mtwivila Bw Victor
Mushi akijibu maswali ya wapiga kura wake katika mkutano huo wa
CCM Iringa mjini leo
CHAMA
cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimeanza kufufua
matumaini ya wananchi wa jimbo la Iringa mjini juu ya kero
zinazowakabili kwa kuwaweka kitimoto madiwani wake katika mkutano wa
hadhara kwa kumtaka kila mwananchi kumhoji diwani wake kama
anatosha ama hatoshi kuendelea kuwaongoza.
Huku
wananchi wa jimbo hilo la Iringa mjini wakikitaka chama hicho
kusaidia kukinusuru chama na kura za chuki kutokana na shirika la
ugavi wa umeme nchini (TANESCO) kuendelea kupandisha gharama za
umeme.
Wakihoji
katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa
Mwembetogwa leo ,wananchi hao walisema kuwa ili CCM jimbo hilo
na Tanzania kwa ujumla kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2015 na ule wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema
mwaka huu ni lazima gharama za umeme ishuke
Kwani
walisema kuwa hatua ya TANESCO kuendelea kuongeza bei ya umeme
ni kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania na kuwa ushindi wa CCM
utatokana na utetezi wa chama katika kuwaondolea mzigo wa bei ya
umeme watanzania.
Mbali
ya hilo pia wananchi wa kata ya Kihesa walimbana diwani wao Bw
Mussa Wanguvu kutokana na hatua ya kushindwa kupigania wananchi
ambao wanatakiwa kuvunja nyumba zao ambazo zimejengwa katika eneo
la Semtema Majengo mapya eneo ambalo halitakiwi kisheria
Diwani Wanguvu akijibu swali hilo alisema kuwa
eneo hilo lilizuiwa baada ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara hasa
wale ambao wamejenga katika mlima na wapo hatarini kuangukiwa na
mawe ila baadhi ya maeneo ambayo si rasmi ni waliachiwa .
Kwa
upande wao wananchi wa kata ya Mtwivila walimtaka diwani wao Bw
Victor Mushi kueleza ni lini atatekeleza ahadi yake ya zahanati na
ubovu wa barabara katika
eneo la Mkimbizi pamoja .
Kwa
upande wake diwani Mushi kuhusu suala la ujenzi wa kituo cha
afya alisema kuwa ahadi hiyo haikuwa ya kwake ila ilikuwa katika
ilani ya CCM japo alisema ujenzi wa mradi huo upo mbioni baada
ya kumaliza miradi ya zamani utaanza mradi huo wa ujenzi wa kituo
cha afya.
Kuhusu
barabara alisema kuwa kata hiyo wamejitahidi kutengeneza mifereji
na zaidi ya Tsh bilioni 1.8 zitatengeneza barabara ya lami kutoka
Mtwivila kwenda Mkwawa na tayari zoezi hilo linaendelea.
Katika
hatua nyingine
Mushi alipinga madai ya wananachi kuwa uongozi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa umekuwa ukifanya usafi katika mji kutokana na
kuwepo kwa ugeni ama vikao kuwa jambo hilo si kweli na kuwa
linafanyika kulingana na bajeti na ufinyu wake.
Katibu
wa CCM wilaya ya Iringa mjini Hassan Mtenga alisema kuwa lengo la
kuwaweka kitimoto madiwani ni kutaka kukata mzizi wa fitina na
kuanzisha utaratibu
mpya wa CCM kutekeleza ilani yake pamoja na kupokea kero za
wananchi.
Hata
hivyo alisema utaratibu huo utaendelea kama njia ya kukiwezesha
chama hicho kuweza kupata ushindi wa kimbunga katika chaguzi
zijazo.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa
Aman Mwamwindi akijibu kero mbali mbali akianza na Hospital ya wilaya
ya Iringa mjini alisema kuwa Hospital hiyo imeendelea kutoa huduma .
Huku ujenzi wa barabara za lami
katika mji huo kupitia pesa za benk ya Dunia alisema barabara
itajengwa kuanzia Samora ,Hospital ya Frelimo , Itamba na maeneo
mengine ya mji .
Kuhusu suala la usafi alisema kuwa
moja kati ya sababu zilizopelekea mji wa Iringa kutoshika nafasi ya
kwanza ni kutokana na hadhi ya makaburi na ndio sababu makaburi ya
makanyangio kuanza kuzungushiwa uzio ili siku moja Manispaa ya
Iringa iweze kushika nafasi ya kwanza .
Alisema kuwa ni vema suala la
maendeleo ya mji wa Iringa lisifanyike kwa itikadi za vyama na
badala yake kufanyika kutokana na mazingira yaliyopo .
Kuhusu suala la Stendi ambalo
limeendelea kuleta lugha mbali mbali kutoka serikalini na viongozi wa
kisiasa alisema kuwa hashangai na kauli za upotoshwaji juu ya ujenzi
wa stendi hiyo ya kisasa ya mkoa itakayogharimu zaidi ya Tsh bilioni 4
fedha kutoka benki ya dunia .
Alisema kuwa mchakato wa ujenzi wa
stendi hiyo umeshirikisha wadau wote nyeti hadi mshauri wa mambo
ya kimazingira kimataifa na tayari ameifanya kazi hiyo na kutoa
maelekezo yake ya kitaalam ambapo ameruhusu ujenzi huo.
Alisema inapojengwa stendi hiyo kutoka
ukingo wa mto ni mita zaidi ya 700 wakati sheria ya ujenzi ya Rufiji na
Iruwasa ni mita kati ya 50 na 60 hivyo stendi hiyo ipo mbali zaidi
kuliko sheria.
Alisema kuwa fedha za ujenzi wa
stendi hiyo hata kama Halmashauri ingekusanya isingeweza kupata fedha
hizo ambazo hata kama ingekusanya kwa miaka zaidi ya 3 bila kupata .
Alisema kuwa wanaotumia maendeleo kwa
ajili ya kutafuta umaarufu katika siasa ni kutowatendea haki wananchi
ambao unawatumikia na kuwa suala la uongo halikubariki katika dini
zote .
Hata hivyo Mwamwindi alisema jitihada
mbali mbali zinazofanywa na serikali ya CCM katika manispaa ya
Iringa ni kutaka kuiwezesha Halmashauri hiyo kuja kuwa jiji kama
ilivyo Mbeya, Mwanza na Arusha .
Hivyo alisema tayari jitihada mbali
mbali za kuwezesha mji wa Iringa kuwa jiji na tayari wamepeleka
mradi wa maji Nduli mradi ambao wakati wa kuwekeana saini mbunge wa
jimbo la Iringa mjini alipata kushiriki .
"Tumepeleka barabara kutoka Tumaini
kwenda Kigonzile KM 6 tumepeleka mabati kwa ajili ya choo mgongo
pamoja na kuweka vituo katika eneo la Kigonzile ili kupeleka huduma
hiyo kwa wananchi ... kwa hiyo ndugu zangu mheshimiwa Mushi
amezungumzia barabara ya kutoka Mkimbizi hadi bima kiasi cha
mabilioni ya fedha ambazo binafsi sijapata kusaini fedha nyingi
kiasi hicho ....sasa tumeanzisha mkakati wa kugawa viwanja na
kupasua njia na ninasema kuwa ujenzi wa stendi upo pale pale na suala
hili lipo kwa waziri mkuu ambaye ndie mwenye TAMISEMI"HABARI NA PICHA KWA HISANI YA FRANSIS GODWIN
No comments:
Post a Comment