Umati
wa wananchi wa makete wakimsikiliza Dkt Slaa wakati akiwahutubia katika
mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya mabehewani
Licha ya kunyesha mvua kubwa, lakini wananchi wa Makete waliendelea kuwasikiliza viongozi hao wa chadema wakihutubia
Helkopta waliyotua nayo viongozi hao wa CHADEMA
Katibu mkuu wa CHADEMA Taifa Dkt Wilbrod Slaa akiwasili viwanja vya mabehewani Makete
Dkt Slaa na viongozi wengine wa CHADEMA wakiingia kwenye helikopta yao tayari kuondoka kuelekea Mbeya
Katibu wa chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa mh. Dk.Wilbrod Slaa jana mchana amehutubia mamia
ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mabehewani wilayani Makete mkoani Njombe
Akizungumza na wakazi wa
wilaya ya Makete Dk.Slaa Katika kutekeleza Oparesheni M4C pamoja Daima katika
eneo la Mabehewani Makete Mjini amewashukuru wananchi kwa ushiriki wao katika uandaaji
wa Rasimu ya Katiba mpya kwa kadri ya uwezo wao
Katika oparesheni hiyo ambayo
ilianza hapo jana kufanyika na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika mkoa
wa Ruvuma amesema kuwa mambo makuu ambayo
yanazungumzwa ni Rasilimali zilizopo hapa nchini pamoja na mchakato wa Katiba mpya ambao unaendelea sasa hapa nchini
Katika Mkutano huo Slaa
aliweza kuongozana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mh. mchungaji Peter Msigwa ambaye
alipata fursa ya kuzungumza na wanamakete ambapo amezungumzia kuhusu uhaba wa
huduma za afya ikiwemo upungufu wa dawa, kushuka kwa kiwango cha elimu
pamoja na sekta zingine
Hata hivyo wananchi
walipozungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti kuhusu ujio wa Viongozi hao wa
Chama wamesema kuwa hii inaleta changamoto kubwa kwa serikali katika kuchochea
Maendeleo kwa wanajamii pamoja na kuongeza kukua kwa uchumi katika nchi
yetu
Viongozi hao wa chadema walielekea mkoani Mbeya kuendelea na ziara yao
No comments:
Post a Comment