Bomu lililotegwa ndani ya gari
limelipuka nje ya makao makuu ya polisi katika mji mkuu wa Misri, Cairo
na kuwauwa zaidi ya watu wanne huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa kulikuwa pia na ufyatulianaji wa risasi.Mlipuko huo umeharibu jengo la makavazi ya sanaa ya kiislamu lililopo karibu na eneo hilo.
Baadaye kulitokea mlipuko mwingine katika kituo cha basi eneo la Dokki na kusababisha vifo zaidi.
Duru zinasema kuwa watu wawili waliojihami kwa bunduki waliwashambulia walinzi katika jengo hilo la polisi.
Kituo cha televisheni cha Serikali kimesema kuwa milio ya risasi ilisikika mara tu baada ya mlipuko huo.
Moshi ulionekana ukifuka juu ya majengo katikati mwa mji na picha za televisheni zilionyesha uharibifu mkubwa wa majengo hayo.
Zaidi ya ambulansi 30 zimepelekwa eneo hilo kushughulikia waathiriwa. Mlipuko huo umetokea siku ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Hosni Mubarak.
No comments:
Post a Comment