Mkuu wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya akizungumza wakati akikagua jengo hilo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo. Kulia ni mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Sumbawanga Vijijini ndugu Mtapima na katikati ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga.PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA KALAMBO Mhandisi wa ujenzi wa wilaya ya Kalambo Issa Liyanga akimuonesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya alipokagua jengo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kasanga wilayani Kalambo.
PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA KALAMBO
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Mkuu
wa mkoa wa Rukwa injinia Stella Manyanya (kulia) akizungumza wakati
akikagua jengo hilo la bweni la wasichana katika shule ya Sekondari
Kasanga wilayani Kalambo. Pembeni yake ni Mhandisi wa ujenzi wa wilaya
ya Kalambo Issa Liyanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya
ya Kalambo Philbert Ngaponda. PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI
WILAYA YA KALAMBO
……………………………………………………………………………….
NA RAMADHANI JUMA,
OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO
MKUU
wa mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya ameziagiza Halmashauri zote
Mkoani hapa pamoja na taasisi nyingine za serikali kutotoa kazi yoyote
ya ujenzi kwa kampuni ya ujenzi ya ‘Juin Constructions Company Limited ’
kutokana na kampuni hiyo kuonekana kufanya kazi zake chini ya kiwango.
Alitoa
maamuzi hayo wakati alipokuwa akikagua jengo la bweni la wasichana
linalojengwa katika shule ya sekondari ya Kasanga iliyopo kata ya
Kasanga wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa .
Alisema
wakandarasi wengi wamekuwa wakiihujumu mikoa ya pembezoni mwa nchi
ukiwemo Mkoa wa Rukwa kwa kujenga miradi isiyo na viwango kwa muda mrefu
sasa, na kwamba umefika wakati wa kupambana na hali hiyo.
Aliagiza
kampuni hiyo iwekwe kwenye orodha ya makampuni yasiyotakiwa kupewa
kazi katika mkoa wa Rukwa mara moja ili iwe fundisho kwa makampuni
mengine yanayolipwa fedha za umma kwa kazi zilizo chini ya kwango.
Mbali
kutekeleza jengo hilo chini ya kiwango, Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema
mkandarasi huyo amekuwa hafuati ushauri wa wataalam wa Halmashauri ya
Kalambo iliyompa kazi hiyo.
“Mkandarasi
huyu hajawahi kupatikana katika eneo la mradi wakati wa ukaguzi hata
siku moja..kila mara wakaguzi wakitembelea mradi huu yeye huwa hayupo
kwahiyo huyu hatufai katika mkoa wetu” alifafanua.
Kwa
upande wake mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Issa
Liyanga alisema wamekuwa wakimsimamia mkandarasi huyo katika hatua
mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo ambapo hata hivyo amekuwa na
ushirikiano hafifu katika kuzingatia ushauri unaotolewa.
No comments:
Post a Comment