Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 18, 2014

MTIBWA YAIPIGA SIMBA GOLI 1 KWA BILA







MTIBWA Sugar imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa kirafiki kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo.

Simba walikuwa wa kwanza kubisha hodi kwenye lango la Mtibwa Sugar kwenye dakika ya 12 lakini shuti la mshambuliaji mpya wa timu hiyo Ally Badru liliishia mikononi mwa kipa Hussein Sharif. Kabla ya kupiga shuti hilio dhaifu Badru alikuwa amepata pasi ya Said Ndemla.

Mtibwa Sugar walijibu mapigo kwenye dakika ya 25 lakini mshambuliaji wake Jamal Mnyate alikosa bao la wazi kwa shuti alilopiga kutoka pembeni kidogo ya lango la Simba.
Timu hiyo kutoka mkoani Morogoro ilitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza nusura wapat bao kwenye dakika ya 27 lakini beki wa Simba Gilbert Kaze aliokoa mpira uliokuwa unatinga wavuni wa mshambuliaji Masoud Ally.

Simba walifanya shambulizi la kushtukiza lakini mshambuliaji wake Betram Mwombeki alipoteza nafasi nzuri ya kufunga  kwenye dakika ya 33 akiwa peke yake na goli lakini shuti lake lilitoka pembeni kidogo ya lango la Mtibwa Sugar. 

Dk 46 Simba walifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Nassoro Masoud’Cholo’ na Adyoun Saleh badala ya Omary Salum na Wiliam Lucian huku Mtibwa wakifanya mabadiliko kwa kumuingiza Vicent Barnabas badala ya Ally Mohamedi aliyeumia.

Dk 53 Mtibwa Sugar walipata pigo baada ya mchezaji wake Salim Mbonde kutolewa nje baada ya kugongana na kipa wake Hussein Shariff na kulazimika kubebwa kwa machela kupelekwa chumba maalumu cha matibabu.
Dk 65 Ally Masoud aliifungia Mtibwa Sugar bao la kuongoza baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Hussein Ramadhani.

Vikosi Simba Yaw Berko. Wiliam Lucian, Omary Salum, Kaze Gilbert, Donald Musoti, Awadh Juma, Ramadhani Chombo, Edward Cristopher, Betram Mwombeki, Ally Badru na Saidi Ndemla.

Mtibwa Hussein Sharif, Said Mkopi, Paul Ngalema, Salim Mbonde, Salvatory Ntebe, Shaabani Nditi, Ally Shomary, Masoud Ally, Juma Luizio, Jamali Mnyate.CHANZO http://pallangyor.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment