Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 5, 2014

RAIS KIKWETE NA MAKAMU DKT. BILAL WAWAONGOZA WANANCHI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. MGIMWA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR.


 Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
PICHA NA MATUKIO BLOG
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
  Mawaziri wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. William Mgimwa wakati likipakiwa kwenye gari tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa ndege kuelekea mkoani Iringa kwa maziko.
 Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho.
 Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, heshima za mwisho.
 Baadhi ya Mawaziriki wakiwa katika foleni kuelekea kutoa heshima zao za mwiho.
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika shughuli hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria shughuli hiyo.
 Baadhi ya Wabunge waliohudhuria shughuli hiyo.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.

No comments:

Post a Comment