Mbali
ya Azam FC timu nyingine zilizofanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali
jioni ya leo ni URA na KCC zote za Uganda baada ya kupata ushindi dhidi
ya KMKM NA Tusker ya Kenya katika michezo yao ya robo fainali.
URA
imewafunga mabingwa wa Zanzibar KMKM bao 1 kwa 0 ambapo bao hilo pekee
na la ushindi limefungwa na Owen Kasule dakika ya 42 Uwanja wa
Gombani, Pemba wakati KCC imeitoa kwa mikwaju ya penalti 4 kwa 3 dhidi
ya Tusker kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa
Amaan, Zanzibar
Kipa
wa KCC, Omar Magoola alipangua penalti mbili ya Ismail Dunga na Luke
Ochieng, wakati za Clifford Alwanga, Brian Osumba na kipa mwenzake
Samuel Odhiambo zikitinga nyavuni.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Waliofunga
penalti za KCC ni Tony Odur, Habib Kavuma, Stephen Bengo na kipa Omar
Magoola na kwa matokeo hayo, KCC itamenyana na Azam FC katika Nusu
Fainali ya kwanza kesho kutwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar Saa 10:00 jioni.
Robo
Fainali ya mwisho imemalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan baada ya
wekundu wa Msimbazi Simba SC kuifunga Chuoni mabao 2-0,mabao hayo
yamefungwa na Ramadhan Singano,kwa ushindi huo Simba itacheza na URA
katika Nusu Fainali ya pili kesho kutwa Saa 2:00 Usiku.
No comments:
Post a Comment