Mh. Spika Anne Makinda akishukuru baada ya kukabidhiwa nakala ya
Katiba ya Jumuiya ya Watanzania
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Makinda ametembelea makazi ya Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Mhe. Modest
Mero, kumsalimu na pia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa
Jumuiya ya watanzania waishio Uswisi. Mh. Spika pamoja na ujumbe wake
alikuwa Geneva, 27-28 Januari 2014, kuhudhulia kikao cha kwanza cha
kamati ya Maspika kwa ajili ya kuandaa mkutano mkuu wa Dunia wa Maspika.
Picha ya pamoja, Mh. Modet Mero, Mh. Anne Makinda na mama Mero,
kwenya makazi ya balozi.
Mh. Spika katika picha ya pamoja na Mh. Balozi Modest Mero na
viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uswisi.
Source Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment