Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 5, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


DV7A3218
WILAYA YA MBEYA MJINI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
    KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 04.01.2014 MAJIRA YA SAA 10:55HRS HUKO MAENEO YA MLIMA NYOKA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, BARABARA YA MBEYA/IRINGA. GARI T.437 AQW AINA YA TOYOTA COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA ANUANI YAKE LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE ASHURA D/O MWINUKA, MIAKA 22, MKINGA, MKAZI WA UYOLE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU

TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WILAYA YA RUNGWE – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 04.01.2014 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO MTAA WA IGOGWE TUKUYU MJINI, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA RAYMOND S/O EMMANUEL, MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIWIRA ROAD TUKUYU MJINI AKIWA NA BHANGI KETE 364 NA MISOKOTO 10 SAWA NA UZITO WA KILO 01 NA GRAM 820. BHANGI HIYO ALIIFICHA KATIKA MIFUKO YA RAMBO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUWAFICHUA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[AHMED. Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment