Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, January 10, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DV7A3218WILAYA YA RUNGWE – MAUAJI. 
MNAMO TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILENGE, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA  RUNGWE  MKOA WA MBEYA. MAGRETH D/O IJUMBA, MIAKA 55, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ILENGE ALIUAWA AKIWA NYUMBANI KWAKE KWA KUPIGWA JIWE KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA KUTUPWA KATIKA SHAMBA LAKE LA MIGOMBA UMBALI WA MITA 69 KUTOKA NYUMBANI KWAKE. MBINU NI KUVUNJA MLANGO WA NYUMBA YA MHANGA AMBAYE ANAISHI PEKE YAKE KUINGIA NDANI NA KUMUUA KWA KUTUMIA JIWE. AIDHA WATU HAO PIA WALIKWENDA MTAA WA PILI NA WALIMSHAMBULIA KISA W/O EPHRAIM, MIAKA 50, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ILENGE KWA KUTUMIA JIWE KICHWANI NA AMELAZWA HOSPITALI YA  MISHENI IGOGWE.  CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHA KUAMINI IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO MLIMA NYOKA, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA, WATU WAWILI 1. CHARLES S/O LIVINGSTONE, MIAKA 32, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA ITEZI NA 2. TATIZO S/O MBWIGA, MIAKA 27, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA WALISHAMBULIWA  KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA MAWE HADI KUFA.  CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI WA PIKIPIKI T.693 CBD AINA YA SHANLEY MALI YA KEVEN S/O MSEMWA, MIAKA 24, MUWANJI, MKULIMA, MKAZI WA UYOLE.  MAREHEMU  CHARLES S/O LIVINGSTONE ALIKUWA ANATOKA MAHAKAMA YA  MWANZO UYOLE AKIWA MLALAMIKAJI KATIKA KESI CC 568/2013 KOSA SHAMBULIO AKIWA NI MLALAMIKAJI NA MAREHEMU TATIZO S/O  MBWAGA  ALIKUWA ANAMSINDIKIZA NA WALIPOFIKA ENEO LA UYOLE KATI WALIIBA PIKIPIKI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO MBALIZI KATA YA BONDE LA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA GEOFREY S/O SACKSON, MIAKA 23, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI AKIWA NA BHANGI KETE 27 SAWA NA UZITO WA GRAM 135. MTUHUMIWA NI MUUZAJI /MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA AU MWENYE KUONA VIASHIRIA VYOVYOTE VYA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBARALI – KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI. 
MNAMO TAREHE 09.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KWATWANGWA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA, TARAFA YA  RUJEWA, WILAYA YA  MBARALI, MKOA WA MBEYA. ASKARI WANYAMAPORI [TANAPA] WAKIMKAMATA  JUMA S/O KALINDI, MIAKA 72, MSUKUMA AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI PEMBE MBILI ZA DIGIDIGI NA NYAMA YA  TEMBO. THAMANI BADO KUFAHAMIKA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII KUACHANA NA TAMAA ZA MALI KWA KUTUMIA NJIA ZISIZO HALALI NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI HALALI ILI WAJIPATIE KIPATO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU WA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UWINDAJI HARAMU ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment