Young Killer Msodoki, rapper mwenye umri
mdogo aliyefanikiwa kuiteka Tanzania na hata kuifikisha sauti yake
Marekani na kumpata shabiki ‘mzungu’ aliyejirekodi na kuweka ujumbe wake
youtube kueleza jinsi anavyomkubali, sasa amefanikiwa kuishi ndoto yake
ya kujiendeleza kimasomo.
Rapper huyo ambaye hivi karibuni alieleza
wazi kuwa anahitaji msaada wa kifedha ili aweze kurudi shule, ameingia
rasmi darasani kusomea Information Technology (IT).
“Am..back…class…”, ameandika Instagram na
kupost picha inayomuonesha akiwa anasoma huku ana headphone shingoni
(Muziki na Shule).
Young Killer amejiunga na chuo kiitwacho
‘Green Pasture’ wiki mbili zilizopita. Kuanzia katikati ya mwaka jana,
Young Killer alianza kuweka wazi wazo lake la kutaka kurudi shule na
aliwahi kutaja masomo ya IT kuwa ndiyo ambayo angependa kusomea.
Tunamtakia kila la kheri kwa hatua nzuri aliyoipiga.
SOURCE: http://www.timesfm.co.tz
No comments:
Post a Comment