Lakini katika orodha ya Etoile du Sahel, ambayo Mwanaspoti imepata nakala yake jana Ijumaa ni kwamba klabu hiyo imepeleka CAF majina 24 tu, na hakuna jina la Emmanuel Okwi.
Iwapo ikitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Etoile inaweza kuongeza majina sita kwani kila klabu inaruhusiwa kutuma majina 30.
Kwa kifupi ni kwamba, Etoile du Sahel haiwezi kumtumia Okwi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa Yanga wanaweza kumtumia raia huyo wa Uganda kwani wametuma jina lake katika shirikisho hilo mjini Cairo, Misri.
Etoile kwenye usajili wake wa CAF imepeleka wachezaji 24 ambao pia hakuna jina la Okwi.
Waliosajiliwa CAF ni Aymen Mathlouthi, Saif Ghezal, Ghazi Abderrazzak, Radhouene Felhi, Marouene Tej, Hamza Lahmar, Alaya Brigui, Baghdad Bounedjah, Abdel Fadel Suanon, Issam Jebali, Franck Kom, Ahmed Mortadha na Ben Ouannes.
Wengine ni Hamouda Chatti, Marouene
Troudi, Hamdi Nagguez, Aymen Ben Ayoub, Drame Michailou, Mohamed Slama,
Zied Essoussi, Rami Bedoui, Aymen Trabelsi, Fehmi Kacem, Khaled Yahia na
Youssef Mouihb
Ingawa, TFF imesimamisha kwa muda Yanga kumtumia Okwi, lakini jambo hilo inaelekea linakosa nguvu baada ya Etoile kuliondoa jina la mchezaji huyo CAF.
Yanga itacheza na Komorozine ya Comoro katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi ujao ikianza Dar es Salaam kabla ya kurudiana Comoro.
Okwi alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea SC Villa ya Uganda kwa mkataba wa miaka miwili huku ikidaiwa kuwa alipewa dola 100,000 (Sh 160 milioni).
SC Villa iliruhusiwa na Fifa kumtumia mchezaji huyo kwa mkataba wa miezi sita wakati sakata la madai ya mishahara na marupurupu yake Etoile yakifanyiwa kazi.
Mbali na madai ya Okwi kwa Etoile hata Simba ilikuwa ikidai dola 300,000 ambazo haijalipwa mpaka sasa na kesi ipo Fifa.
Baada ya Okwi kuidhinishwa Villa, Yanga ilikaa na mchezaji huyo pamoja na mwanasheria wake Edgar Agaba ambaye alifuata utaratibu wa kisheria na kuwauzia Jangwani mchezaji huyo ambaye mpaka sasa ameifungia mabao matatu kwenye michezo ya kirafiki.
Lakini TFF imezuia usajili wake, ikitaka ufafanuzi zaidi kutoka Fifa juu ya uhalali wa Yanga kumtumia mchezaji huyo ambaye alikuwa ameidhinishwa kwa muda Villa.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema juzi Alhamisi kuwa klabu yake haina tatizo na Okwi ila wanataka kulipwa haki zao kutoka Etoile pamoja na aslimia 20 ya mauzo ya mchezaji huyo.
Yanga kupitia kwa katibu wake, Benno Njovu imedai kwamba kuna hujuma zinafanywa dhidi ya mchezaji huyo ili asiichezee Yanga ingawa TFF wamepinga na kudai ni utaratibu tu wa kawaida.chanzo mwanaspoti

No comments:
Post a Comment