Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akisalimiana na
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Kidegesho.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mahmood Mgimwa akiongea na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Waziri
mpya katika Wizara ya Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu na Naibu
Waziri mpya mh. Mahmood Mgimwa wapokelewa kwa shangwe makao makuu ya
wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.
Wizara ya
Maliasili na Utalii imefanya mapokezi ya Mawaziri wake wapya leo
Jumanne 21 Januari 2014, ambapo watumishi waliopo Makao Makuu ya wizara
wamepata fursa ya kukutana na kufanya maongezi na mawaziri hao.
Mapokezi
hayo yanafuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzanaia Mhe. Jakaya Kikwete wishoni mwa wiki
iliyopita na kufuatiwa kuapisha kwao Jan 20, 2014 katika viwanja vya
ikulu jijini Dar.
Naibu
Waziri Mhe. Mahmood Mgimwa amewaahidi wafanyakazi wa Maliasili na Utalii
kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kuleta maendeleo
ambayo wananchi wanayategemea kutoka katika Wizara hii.
Kwa
upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu
amewakikishia wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya kazi
kwa ushirikiano na weledi ili kuweza kuifanya Wizara kuongeza pato la
Taifa kupitia Utalii.
Aidha,
Mhe Nyalandu amewaasa watumishi wote kudumisha amani na upendo katika
maeneo yao ya kazi ili kujenga mazingira mazuri ya kazi na kuongeza
ufanisi.
No comments:
Post a Comment