Young Africans kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya KS
Flamurtari Vlore inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu
nchini Albania ikiwa ni sehemu ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu
kwa timu zote, mchezo utakaofanyika katika eneo la Side Manavagat.
Huu utakua ni mchezo wa tatu wa Young Africans wa kujipima nguvu
dhidi ya timu hiyo ya Ligi Kuu nchini Albani baada ya kuwa imeshacheza
michezo miwili na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ankara
Sekerspor na 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van Der Plyum ameendelea na mazoezi
leo asubuhi na jioni ataendelea na mazoezi pia kuwaandaa vijana wake
kuwa tayari kwa mchezo huo, lakini pia kuwaweka tayari kwa ajili ya
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Baada ya mchezo dhidi ya timu KS Flamurtari Vlore kesho, Young
Africans itakamilisha ziara yake ya kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa
kucheza na timu ya Simurq PIK inayoshikri Ligi Kuu nchini Azerbaijan
katikati ya wiki ijayo kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini
Tanzania.
Hali ya hewa jijini Manavgat ni nzuri na sio ya baridi kali kiasi
kwamba haiwalazimu wachezaji kuwaa vifaa vya michezo vya baridi kwani
hali inawaruhusu kuweza kufanya mazoezi na kucheza bila kuwa na mataitzo
yoyote.
Mpaka sasa hakuna katika kambi ya klabu ya Young Africans nchini
Uturuki hakuna mchezaji yoyote majeruhi isipokuwa kiungo Hassan Dilunga
ambaye anasumbuliwa na malaria na tayari anaendelea vizuri baada ya
kupatiwa tiba na daktari wa timu Dr. Suphian Juma
No comments:
Post a Comment