Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye alipowasili mapema leo kwenye
makao makuu ya ofisi hizo zilizopo Mikocheni jijini Dar,pichani kati
anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akitoa
maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye kwenye moja
ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea
shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo na urushaji
wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati
anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
Mkuu wa
Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akitoa ufafanuzi mfupi kwa
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye alipotembelea kitengo hicho cha
habari na kujionea uandaaji wa habari ya televisheni na redio
unavyofanyika.
Mmoja wa
Watangazaji kipindii cha Michezo Clouds FM, kiitwacho Sports Extra,
Ibrahim Masoud a.k.a Maestro akifanya mahojiano mafupi na Waziri Mkuu
Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye kuhusiana ushabiki wake mkubwa kwa timu ya
Simba sambamba na migogoro iliyoikumba club hiyo ya Msimbazi
Ruge
Mutahaba akitoa ufafanu mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick
Sumaye,kuhusiana na Kifaa maalum na cha kisasa cha kurushia matangazo ya
biashara,pichani nyuma ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM, Joyce
Shebe akisikiliza.
Waziri Mkuu
Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akiwa kwenye chumba cha kurekodia mahojiano
mbalimbali,akiwa amekutana na wadau wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania (UTT), pichani kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa UTT, Mfaume
Kimario na Afisa Masoko na Uhusiano, Bwa.Rahim Mwanga
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo
mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na
urushaji wa matangazo kwa njia ya kisasa ndani ya studio kuu ya redio
Clouds FM, Sumaye amefanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo na urushaji wa
matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla.
Ruge
Mutahaba akimtambulisha Mkurugenzi mwanzake wa Maendeleo ya Biashara,
Sheba Kussaga kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye
Mkuu wa
Kitengo cha uzalishaji vipindi wa Clouds TV, Bw Kanyopa akitoa ufafanuzi
mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick Sumaye namna ya kuandaa na
kuhariri vipindi vya televisheni.
Ruge
Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mh.Frederick
Sumaye kuhusiana na mitambo ya kisasa ya kurushia matangazo ya
televisheni na ubora wa picha za televisheni unaotoka kwenye mitambo
hiyo ya kisasa.
PICHA ZOTE NA MICHUZIJR WA MICHUZI MEDIA GROUP
No comments:
Post a Comment