skip to main |
skip to sidebar
ZITTO AANIKA UFISADI WA MBOWE,JIONEE HAPA
MBUNGE wa Kigoma
Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameshusha tuhuma nzito dhidi ya
Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, zikimhusisha na ufisadi.
Hata hivyo, Mbowe naye amejibu tuhuma hizo akisema ni busara zaidi kwa
mhusika kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake badala ya kuibua tuhuma
nyingine.
Madai hayo ya Zitto kwa Mbowe ni kilele cha siasa za kuchafuana,
kutukanana na kuvunjiana heshima kilichodumu kwa takribani miezi mitatu
sasa kupitia vyombo tofauti vya habari.
Akiandika katika ukurasa wake binafsi wa facebook jana jioni, Zitto
alisema Mbowe hawezi kumnyooshea yeye kidole kuhusu masuala ya maadili
kwa vile yeye mwenyewe (Freeman) ndiye mvunja maadili namba moja ndani
ya chama hicho.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Jana mchana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, aliwaambia
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba Zitto amepewa magari
mawili na Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono; ambaye ni mmoja
wa watu waliotajwa na chama hicho kama mafisadi.
"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na
Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Mbowe Sh.
milioni 40 ili Mbowe asifanye kampeni Jimbo la Musoma Vijijini.
“Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi
kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman Sh. milioni 20 za uchaguzi wa
Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa.
“Nadhani alimwambia pia kuwa mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe Sh. milioni
200 za Kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa
Mbowe Sh. milioni 100 za kampeni. Lissu anajua....?
“Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu
masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya
kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
“Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni
kifaranga tu. Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia
deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke
wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club
Bilicanas.
“They must know I am not a push over (Ni lazima wafahamu kwamba mimi si
mtu wanayeweza kumchezea wanavyotaka). Chacha (Wangwe) died, I won't
(Chacha Wangwe alikufa, Mimi Hawaniwezi.”
“Mtu ambaye hawezi kuheshimu ...... hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu
maadili," aliandika Zitto katika ukurasa wake wa facebook baada ya Tundu
kutoa tuhuma zake.
Lissu alikuwa akizungumza katika mkutano ambao Chadema ilitangaza
kuwafuta uanachama wanachama wake wawili; Dk. Kitila Mkumbo na Samson
Mwigamba.
Zaidi ya kuwafukuza akina Kitila, chama hicho jana kimewaagiza viongozi
na wanachama wake kutoshirikiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia
chama hicho, Zitto Kabwe.
Zitto alifungua kesi wiki iliyopita akitaka kamati hiyo isijadili
uanachama wake, lakini hatua hiyo ya kamati kuu kuwaagiza viongozi wake
wasishirikiane na Kabwe kwenye masuala ya Chadema, imetafsiriwa kama
kumfanya si mwanachama.
Mwanasheria wa Zitto, Albert Msando, ameliambia gazeti hili jana kwamba
ilichofanya Kamati Kuu (CC) kwenye kikao hicho kuhusu Zitto ni
“kuingilia uhuru wa mahakama” kwa vile tayari wameshampa adhabu wakati
Mahakama inasikiliza shauri lake.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama
hicho jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod
Slaa, alisema wamechukua hatua hiyo kwa sababu wamebaini Kitila na
wenzake walikuwa na lengo la kubomoa Chadema.
“Viongozi hawa walikuwa wameandaa mkakati wa muda mrefu wa kukibomoa
chama kwa kukichafua kwa wananchi na kuwachafua viongozi wa juu kwa
kutumia tuhuma za uongo za ufisadi,” alisema Slaa.
Slaa alikuwa akizungumzia waraka wa siri ulioandaliwa na Kitila na
Mwigamba uliotaka kufanyika kwa mabadiliko katika ngazi ya juu ya
uongozi wa chama hicho.
Majibu ya Mbowe
Akizungumza na mwandishi wetu Mbowe alisema ni utoto kukwepa kujibu hoja
kwa kuanzisha tuhuma dhidi ya mtu mwingine ambazo si za kweli.
“Mimi nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu
tuhuma hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine.
Anapaswa kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.
“Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama
Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni
kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete
au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo
gani?” alihoji Mbowe.
Mbowe alilaumu baadhi ya vyombo vya habari kushiriki kumchafua kwa
taarifa za kutunga kutoka kwa watu anaodhani wamekuwa na uhusiano na
Zitto.CHANZO JF
No comments:
Post a Comment