kiongozi
wa Kanisa la World Message Last Warning ambaye alitabiri kwamba mwaka
2000 utakuwa mwisho wa dunia, Wilson Bushara (53) amefariki dunia.
Bushara
ambaye alivuta vyombo vingi vya habari alipotabiri na kusisitiza kwamba
mwisho wa dunia utakuwa Juni 30 mwaka 1999 na kusashawishi waumini wake
kuuza mali zao na kununua nafasi zao mbinguni alifariki asubuhi ya jana.
Alitabiri na kusisitiza kwamba dunia itafikia mwisho wake kabla ya kuingia kwa milenia mpya, ambayo ilikuwa ni mwaka 2000.
Hata
baada ya tarehe hiyo aliyoitaja kupita bila tukio hilo kutokea, Bushara
alikimbilia mafichoni baada ya polisi kuvamia kambo yake ya maombi ya
Bukoto iliyokuwa huko kwenye Wilaya ya Luweero Jimbo la Nakaseke
Septemba 18, 1999.
Bushara
anatambulika kuwa ana ushirikiano na kiongoni mwingine wa kundi la
kidini, Joseph Kibwetere ambaye aliwashawishi waumini wake zaidi ya 1000
kujichoma moto kanisani Machi 17, 1999.
Hata
hivyo aliamua kukataa kuwa na ushirikiano na Kibwetere pamoja na kuwa na
ushahidi wa picha walizopiga kwenye matukio kadhaa wakiwa pamoja.
Bushera
pamoja na baadhi ya waumini wake ambao wengi walikuwa wakifanya kazi za
kuuza maziwa na uhudumu kwenye hoteli wote walikimbilia wilayani Busia
ambapo walijificha baada ya kusikia taarifa kwamba polisi walikuwa
wakitaka kuwakamata.
Alioa
wake tisa aliokuwa akiishi nao kwa pamoja, mmoja kati yao akiwa binti wa
miaka 15. Miaka 10 baadaye, yaani mwaka 2011 Bushara aliibuka na
kutabiri kwamba dunia inaelekea kufikia mwisho wake siku za karibuni na
kuanza kugawa kadi za mwaliko kwa waumini wake, kwa ajili ya tafrija
maalumu ya "karamu ya mwisho" ambazo kila moja iliuzwa kwa Sh23,000 za
Uganda.
Aliwaeleza
wafuasi wake kwamba ishara za mwisho huo wa dunia ziko wazi ikiwemo
miale mikali ya radi na milipuko ya volcano wanayoishuhudia kwa mwaka
huo ndiyo uthibitisho kwamba dunia imefikia mwisho. Kwa kusisitiza,
aliwahakikishia kwamba wale watakaokuwa wamenunua kadi hizo ndio
watakaopata fursa ya 'kunyakuliwa' moja kwa moja kwenda mbinguni na wale
ambao hawatakuwa wamezipata, wataishia kwenye moto wa jehanamu.
Kwa
wakati huu, Bushara alikuwa makini akikataa kutaja tarehe rasmi ya
mwisho huo wa dunia aliokuwa akiutabiri. Bushara amefariki huku
akikabiliwa na mashtaka kadhaa mahakamani, ikiwemo kufunguwa kanisa lake
ambalo lilipigwa marufuku.
Mei mwaka
jana alishtakiwa kwa ulaghai na kuitisha mkusanyiko usiokuwa halali
kisheria, kisha kushikiliwa kwenye gereza la Luzira na hatimaye
kuachiwa.
CHANZO MWANANCHI
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment