Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 10, 2014

BARCELONA WAICHAPA SEVILA 4 , MESSI APIGA MBILI


Ushindi kwenye mvua: Lionel Messi amefunga mabao mawili jana Barcelona ikishinda 4-1 dhidi ya Sevilla
BARCELONA ya Hispania imerejea kileleni mwa La Liga kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sevilla ugenini jana.
Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Sanchez dakika ya 34, Messi aliyefunga mawili dakika ya 44 na 55 na Fabregas dakika ya 87, wakati bao pekee la Sevilla lilifungwa na Moreno dakika ya 15.
Kwa matokeo hayo, Barca inatimiza pointi 57 sawa na Real Madrid na Atletico Madrid baada ya timu zote kucheza mechi 23, lakini zinapishana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Barca ina mabao 46 zaidi, Real 41 na Atleitco 40- hii inamaanisha mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Hispania mwaka huu ni moto.
At the double: Messi (left) scored twice to help Barcelona to a 3-1 win against Sevilla
Messi (kushoto) akishangilia bao lake la pili jana
NA BIN ZUBERY

No comments:

Post a Comment