Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Kanda ya Ziwa Mashariki leo
kimewavua nyadhifa zao viongozi wake watano wa jimbo la Kahama kwa
makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukiuka taratibu za chama hicho.
Uamuzi
huo umetolewa na Mratibu wa Chedema Kanda ya Ziwa Mashariki Renatus
Nzemo katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya Kanda ya Ziwa
Mashariki na kupitia mazimio hayo kabla ya kutoa uamuzi.
Viongozi
waliovuliwa nyadhfa zao ni Mwenyekiti wa jimbo la Kahama Israel
Barikiel, Katibu wa Jimbo Vicent Kilukilwa, Katibu Mwenezi wa jimbo
Bobson Wambura, Mwenyekiti Bawacha Kasigwa Adram na Mwenyekiti Bavicha
Benedict Shija.
Katika Barua
yake aliyoiandika kwa viongozi hao, Nzemo amesema viongozi hao
wanakabiliwa na tuhuma za kikiuka tamko la kamati kuu ya chama
lililowazuaia wanachama wote kushirikiana na aliyekuwa naibu katika mkuu
wa chama hicho Zitto Kabwe.
Tuhuma
zingine ni kushiriki kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Ubagwe
kupitia chama cha TADEA, huku viongozi hao wakipita na kujinadi kuwa
wako tayari kumfuata Zitto popote atakapokuwa.
Aidha Nzemo
amesema viongozi hao wamekuwa wakitumia nembo ya CHADEMA kunadi chama
kingine cha Alliance for change and Transparency (ACT), kinyume cha
maadili ya CHADEMA katika katiba yake ya mwaka 2006.
Nzemo amesema
kutokana na tuhuma hizo na zile zilizotolewa na baraza la mashauriano
wilaya ya Kahama, viongozi hao wanatakiwa kukabidha ofisi na vifaa vya
chama kwa baraza la wazee jimbo la Kahama mara wapatapo barua hizo.
..Via Dunia kiganjani blog
No comments:
Post a Comment