
Kuna
kila sababu za Barcelona na Real Madrid zikakutana kwenye mchezo wa
fainali ya Copa del Rey baada ya wasakata kabumbu hao wa jiji la
Barcelona kuwachapa Real Sociedad waliokuwa pungufu mabao 2-0 katika
mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Copa del Rey uliopigwa kwenye dimba
la Nou Camp.
Katika
mchezo huo, mlinzi Javier Mascherano alinusurika kuadhibiwa baada ya
kumvuta jezi Carlos Vela muda mchache kabla Sergio Busquets hajaifungia
Barca bao la kuongoza.
Badala yake mchezaji wa Sociedad Inigo Martinez alioneshwa kadi nyekundu kwa mchezo usiokuwa wa kiungwana.









No comments:
Post a Comment