Aziza
Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi
sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo
mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai.
Aziza
Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi
sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo
mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai.
Nyumba
ambayo familia ya Aziza Maohamed ilikuwa ikiishi awali kabla
ya kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua katika kitongoji
cha Kijweni kijiji cha Mijongweni kata ya Machame/Weruweru.
Sehemu ambayo analala kwa sasa mtoto wa Aziza Mahamed,Sikujua Aloyce.
Nyumba ya familia ya Aziza Mohamed iliyoezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita wilayani Hai.
Misaada toka Bonite bottlers ikishishwa
Mabati yakishushwa kijijni hapo
Mkuu wa
kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers Christopher
Loiruk akikabidhi msaada wa bati na chakula kwa mkuu wa wilaya ya Hai
,Novatus Makunga kwa ajili ya wahanga wa mvua iliyoambatana na upepo
iliyoezua paa za nyumba huku kaya zaidi ya 1000 zikikosa makazi na
chakula
Mkuu wa
kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers Christopher
Loiruk akikabidhi msaada wa bati na chakula kwa mkuu wa wilaya ya Hai
,Novatus Makunga kwa ajili ya wahanga wa mvua iliyoambatana na upepo
iliyoezua paa za nyumba huku kaya zaidi ya 1000 zikikosa makazi na
chakula
Choo hicho kinavyoonekana kwa nje.
Hali mbaya
Mkuu wa
wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akiteta jambo na katibu wa mbunge wa
jimbo la Hai,Richard Mtui.Kulia kwa ni mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Hai,Merikizedeck Humbe.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.
FAMILIA
moja ya watu watatu akiwemo mtoto wa umri wa miaka saba imelazimika
kuhamishia makazi chooni baada ya paa la nyumba waliyokuwa wakiishi
kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita
katika wilaya ya Hai.
Familia
hiyo ya Aziza Mohamed (55) mwanae wa kiume, Sikujua Aloyce (40) na
mjukuu wake wakazi wa kitongoji cha Kijiweni kijiji cha Mijongweni kata
ya Machame Weruweru imekuwa ikiishi kwa zaidi ya siku 14 katika choo
hicho ambacho paa lake lilisalimika wakati mvua hiyo ikinyesha.
Akizungumzia
tukio hilo Aziza alisema wakati mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali
ikinyesha alikuwa ametoka nyumbani kwake na kwamba baada ya kuona hali
imekuwa mbaya akalazimika kukimbia kurudi nyumbani.
"Mvua
ilivyokuja nilikuwa sipo nilivyoona hali imekuwa ni mbaya na upepo
uliokuwepo ikabidi nikimbilie nyumbani ,nikaanza kumtafuta huyu mtoto na
baba yake,nikawa na tangatanga nataka nipike sasa vile nashangaa
shangaa kutaka kujua mtoto yuko wapi nikaona kidogo nyumba inafunuliwa
bati nikiwa humo humo ndani."alisema Aziza.
"Kumbe
mtoto na baba yake walikuwa wako chumba cha pili Nyumba kubwa ndipo
baadae nikamsikia mtoto ikabidi nianze kupiga kelele tokeni huko tokeni
huko,ndio wakatoka ikabidi tukimbilie huku chooni tukaja kupumzika mpaka
mvua ikaisha ambako tunaishi hadi sasa."aliongeza Aziza.
Alisema
hivi sasa choo hicho wamekuwa wakikitumia nyakati za mchana kwa ajili ya
kujisaidia na kwamba ifikapo usiku hulazimika kufunika shimo la choo
hicho kwa gunia ,na kisha kuweka matandiko kwa ajili ya kulala.
Mengi,Mbowe watoa msaada wa chakula na bati.
Mwenyekiti
mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi kupitia kampuni tanzu ya
Bonite Bottlers ya mjini Moshi ametoa msaada wa mabati 200,kilogramu
2500 za unga pamoja na kilogaramu 100 za maharage kwa ajili ya kusaidia
familia zilizo athirika na mvua hizo.
Akikabidhi
msaada huo juzi mkuu wa kitengo cha mauzo na masoko wa kampuni ya
Bonite Bottlers Christopher Loiruk alisema Mwenyekiti wa makampuni ya
IPP,Mengi pamoja na uongozi wa kiwanda umeguswa na tatizo hilo kwa kuona
kuwa walioathirika ni watanzania wenzetuhivyo hawana budi kupatiwa
msaada.
"Kama
Bonite Bottlers na Mwenyekiti wetu ,Reginald Mengi tumeguswa na tatizo
hili kwa kuona kuwa hawa ni Watanzania wenzetu,wana Kilimanjaro
wenzetu,ndugu zeti na tunafahamu matatizo hayapigi hodi, kwa hiyo
yanapotokea ni lazima sote tuoneshe uzaledo ili tuweze
kusaidiana"alisema Loiruk.
"Tumeanza
kwa kutoa mabati 200,tuna vyakula unga kilo 2500,na maharage kilo 100
tunaomba muwakilishe kwa waathirika ,tunaomba makampuni mengine na hata
watu binafsi waweze kuja kuwasaidia hawa watu ambao hawana mahala pa
kukaa na hata chakula."aliongeza Loiruk.
Kwa
upande wake katibu wa mbunge wa jimbo la Hai,Richard Mtui alisema Mbunge
wa jimbo la Hai ,Freeman Mbowe tayari amekabidhi bati 26 kwa familia
zilizofikwa na tatizo hilo huku akiahidi kutoa kiasi cha sh milioni 7
ambapo sehemu ya fedha hizo zinatoka katika mfuko wa jimbo wa Mbunge .
No comments:
Post a Comment