Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SSP.Cordula Lyimo, akitoa taarifa
kwa waandishi wa habari leo juu ya kukamtwa kwa meno ya Tembo vipande 16
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 17 milioni.Vipande hivyo
vimekamatwa februari 16 mwaka huu saa tano usiku kwenye kizuizi cha
mazao cha kijiji cha Ukimbu wilaya ya Manyoni. Siku nne
zilizopita,vipande vingine 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya
shilingi 43 milioni,vilikamatwa eneo hilo hilo.(Picha na Nathaniel
Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI
la Polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata vipande 16 vya meno ya
ndovu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 17.
Meno
hayo yamekamatwa siku nne (12/2/2014) toka meno mengine vipande 21
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 43 milioni, kukamatwa kwenye eneo
lile lile la kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha Ukimbu kata
ya Mgandu wilaya ya Manyoni.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa
Singida.SSP.Cordula Lyimo amesema meno hayo yamekamatwa febr.16 saa tano
usiku huko katika kizuizi cha mazao kilichopo katika kijiji cha
Ukimbu,kata ya Mgandu tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni.
Amesema askari wakiwa katika kizuizi hicho,walifanya ukaguzi kwenye gari T.288 AJF aina ya scania mali ya kampuni ya super service likiendeshwa na dereva Ally Hamadi, likitokea Makogorosi Chunya,likielekea Itigi wilaya ya Manyoni.
“Baada
ya upekuzi huo,walikuta meno hayo yakiwa yamehifadhiwa ndani ya begi la
nguo na kuwekwa kwenye keria za ndani ya basi.Mtuhumiwa aliweza
kupatikana wakati akiwa katika juhudi za kutaka kutoka nda ya basi ili
akimbie”,amesema Lyimo.
Kaimu
kamanda huyo,amesema uchuguzi zaidi unaendelea ili kubaini au kupata
mtandao kamili unaojihusisha na kuwinda pamoja na kununua nyara hizo.
No comments:
Post a Comment