Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) akiangalia takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania.
Anayemuonesha ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Bibi Mariam Khan (Wa
pili kulia) aliyembelea Ofisi za Tume ya Mipango leo. Wengine pichani ni
Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu),
Bibi Florence Mwanri (Kushoto), Mchambuzi Mkuu wa Sera, Bw. Edwin Ninde
(Wa pili kushoto) na Mtaalam wa Masuala ya Idadi ya Watu toka UNFPA,
Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu.
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Idadi ya Watu (UNFPA), Bibi Mariam Khan leo alitembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na kutoa wito kwa serikali kufanya hima katika kukabiliana na changamoto za ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa mijini nchini Tanzania.
Hata
hivyo, Bibi Khan alisema kuwa licha ya kuwa ongezeko la idadi ya watu
linaathari mbalimbali kama lisipothibiwa, Tanzania inaweza kutuma fursa
hiyo kwa kuwekeza kwa vijana kama nguvu kazi kwa shughuli za kimaendeleo
ili kuongeza pato na uchumi wa taifa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip
Mpango alisema kuwa serikali inatambua changamoto hizo, na kuwa kwa
sasa inajipanga kuipitia Sera ya Idadi ya Watu ya Mwaka 2006 ili iendane
na changamoto hizo.
Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence
Mwanri (Kushoto) akifuatilia kwa makini takwimu zinazohusiana na
masuala ya idadi ya watu nchini Tanzania zilizokuwa zikiwasilishwa na
Bibi Mariam Khan (hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Tume ya
Mipango. Kulia ni Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango), Bw. Edwin Ninde.Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia)
akiangalia kwa umakini sana takwimu zinazohusiana na masuala ya idadi ya
watu nchini Tanzania. Anayemuonesha ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA,
Bibi Mariam Khan (Kushoto).Mtaalam
wa Masuala ya Idadi ya Watu toka UNFPA, Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu
(Kushoto) akizungumza wakati alipofuatana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa
UNFPA, Bibi Mariam Khan (Kulia) kutembelea Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango
No comments:
Post a Comment