| MILOVAN NA MWENZAKE WAKIWA WAMESHIKA JEZI ZA MYNMAR |
Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic ameula baada ya kupata ajira mpya ya kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Myanmar.
Milovan amethibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu katika nafasi hiyo na tayari yuko nchini humo.
Kocha huyo wa zamani wa Simba atakuwa chini ya kocha mwingine mzoefu, Raddy Avramovic ambaye aliwahi kuwa kocha mkuu wa Singapore mwenye mafanikio makubwa.
Jana
kulikuwa na sherehe maalum iliyofanywa na Shirikisho la Soka la Myanmar
(MFF) kuwakaribisha makocha wote na benchi zima la ufundi akiwemo
Milovan.
“Kweli
sasa niko hapa na mambo yamekwenda vizuri, kazi yetu ndivyo ilivyo ni
safari kila siku, ila ninafurahi kuwa hapa,” alisema Milovan katika
mahojiano na SALEHJEMBE



No comments:
Post a Comment