Baadhi
ya madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana katika mabanda mbalimbali
katika maonesho ya 53 ya Kimataifa ya Bangkok Gems and Jewelry Fair. Mfanyabiashara
wa madini na Afisa Masoko wa Kampuni ya Tom Gems Tanzania, akimwonesha
mgeni aliyefika katika banda la Tanzania kuona madini ghafi ya
Tanzanite yanayozalishwa Tanzania pekee. Wageni wengi wamefika katika
banda hilo kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania. Mwenyekiti
wa Madini ya Viwandani Bw. Kassim Iddi Pazi, akimwonesha mgeni madini
ya Ruby. Kutokana na maelezo ya Bw. Pazi, ameeleza kuwa, madini hayo
yametoka katika maeneo ya Winza Dodoma na Matombo Morogoro. Mfanyabiashara
wa Madini kutoka Kampuni ya Tom Gems Bw.Benjamin Mtalemwa akimwonesha
mgeni madini mbalimbali alipotembelea banda la Tanzania. Wanaoshuhudia
kutoka kulia ni Mthamini wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini
Bw. Edward Rweymamu, Wa pili kulia ni Afisa Madini kutoka Shirika la
Madini Tanzania (STAMICO). Bw. Peter Maha, na wa kwanza kulia ni Afisa
toka Wizarani Bibi. Margareth Muhony.
…………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Bangkok
Madini
ya Tanzanite yamekuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya 53 ya
Kimataifa ya‘’Bangkok Gems and Jewelry Fair’’, yanayoendelea katika eneo
la kibiashara la ‘Impact Challenger’, jijini Bangkok.
Madini
ya Tanzanite yanayozalishwa nchini Tanzania pekee duniani, yamekuwa
kivutio kikubwa kwa wageni wanaotembelea maonesho hayo ikiwemo
wauzaji, wanunuzi na wafanyabiashara ambao wamefika katika banda la
Tanzania kutaka kuona Tanzanite halisi kutoka Tanzania.
Aidha,
pamoja na kwamba madini ya Tanzanite yanazalishwa na Tanzania pekee,
lakini katika maonesho hayo ya Bangkok, madini hayo yanapatikana kwa
kiasi kikubwa katika mabanda ya washiriki kutoka nchi mbalimbali
duniani jambo ambalo linaonesha namna madini hayo yalivyo na muhimu
katika sekta zakibiashara na kiuchumi.
Akizungumzia
suala la uwepo wa madini ya Tanzanite kwa kiasi kikubwa katika soko la
kimataifa, na katika maonesho hayo, Kamishna Msaidizi wa Madini ,
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba, ameeleza kuwa, uwepo
wa Tanzanite katika soko la kimataifa unaashiria mahitaji makubwa ya
madini hayo duniani na umuhimu wake katika kuchangia ukuaji wa uchumi
wa Tanzania, na nchi nyinginezo ikiwemo thamani yake katika soko la
kimataifa na upekee wake.
Aidha, ,
aliongeza kuwa, hiyo ni changamoto katika uthibiti wa madini hayo
katika soko la kimataifa kutokana na uwiano wa takwimu za kiasi cha
madini kinachotoka kwa kufuata taratibu za usafirishaji madini hayo nje
ya nchi na uwingi halisi unaoonekana katika soko la Kimataifa.
“Uwiano
wa takwimu za uzalishaji Tanzania na idadi halisi ya madini iliyopo
katika maonesho ya kimataifa ni tofauti. Hii ni changamoto katika
udhibiti wa madini haya” Amesema Kamishna Komba.
Hivyo,
ameongeza kuwa, Serikali inalifanyia kazi suala hili kwa lengo la
kufanikisha usimamizi na biashara endelevu ya madini ya Vito na usonara.
Mbali
na madini ya Tanzanite kuwa kivutio, katika banda la Tanzania, vinyago
vinavyotengenezwa kutokana na mawe aina ya Zoisite, Basalt,
Limestone, Travertine, Granite na White marbale yanayopatikana Tanzania
ambayo yametengenezwa mapambo mbalimbali ya majumbani yamekuwa kivutio
kikubwa katika maonesho hayo kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania
kutoka nchi za Ulaya na Asia, akiwemo pia Rais wa Shirikisho la
wafanyabiashara wa vito na usonara Bw. Somchai Phornchindarak, ambaye
pia alitembelea Banda la Tanzania na kuonesha kuvutiwa na kushangazwa na
mapambo hayo.
No comments:
Post a Comment