Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda
kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF
ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).TFF
ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo
itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa
miguu.Kamati
hiyo itaongozwa na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali,
Gabriel Nderumaki wakati Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha
Wanawake (TWFA).Wajumbe
ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu, Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard
Kasesela, Boniface Wambura na Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa
kuajiriwa hivi karibuni.
Kamati
itafanya kikao chake cha kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye
hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7 mchana.
KILA LA KHERI YANGA MECHI YA LIGI YA MABINGWA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye
mechi yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi ya Al Ahly kutoka Misri.
Mechi
hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kuanzia 10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini
Cairo, Misri.
Maandalizi
ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda
na waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi
hiyo inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.
Milango
yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa
Ndani (Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa
kuanzia chuo cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari
maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani.
Vilevile washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani
wakiwa na silaha au vifaa vyovyote vya chuma.
MAREKEBISHO YA MECHI VPL, FDL
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya marekebisho madogo ya ratiba kwa
mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na moja ya Ligi Daraja la
Kwanza (VPL).
Mechi
namba 143 kati ya Tanzania Prisons na Simba iliyokuwa ichezwe Machi 8
mwaka huu sasa imesogezwa kwa siku moja hadi Machi 9 mwaka huu, kwa vile
Machi 8 mwaka huu Mbeya City itautumia uwanja huo kwa mechi nyingine ya
VPL.
Nayo
Mgambo Shooting iliyokuwa icheze na Kagera Sugar, Aprili 12 mwaka huu
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga sasa imesogezwa hadi Aprili 13 mwaka
huu kwa vile Kituo cha Tanga kitakuwa na mechi mbili.
Kwa
upande wa FDL, mechi ya Mkamba Rangers na Kimondo SC sasa itachezwa
Machi 3 mwaka huu badala ya Machi 9 mwaka huu mjini Ifakara. Mechi hiyo
imerudishwa nyuma ili kuipunguzia gharama Kimondo SC kwani Machi 1 mwaka
huu itacheza na Burkina Faso mjini Morogoro.
No comments:
Post a Comment