Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 28, 2014

MANISPAA YA KINONDONI YAJIPANGA KUKUSANYA KODI YA MAJENGO



Manispaa ya kinondoni imejipanga kuhakikisha inakusanya fedha nyingi za kodi ya majengo kwa kuweka mfumo rahisi kwa walipaji.Akizungumza katika semina ya iliyohusisha watendaji,wenyeviti wa serikali za mitaa,wahasibu na watu wengine Meya wa manispaa hiyo Mstahiki Yusuph Mwenda amewataka watendaji wake wa kata 34,kufanya kazi yao kwa uaminifu mkubwa ili kupata mapato yatakayosaidia shughuli mbalimbali za maendeleo.

Alisema baada ya mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)Kukubali kuacha jukumu la ukusanyaji wa kodi za majengo kuwa chini ya Halmashauri,kinondoni imejipanga kuweka mfumo rahisi kwa walipaji bila ya kulazimika kwenda ofisi za manispaa kufanya hivyo.

Benki ya CRDB,au kwa wakala wa Maxi malipo ambaye ameunganishwa na mitandao mbalimbali ya simu,pia katika ofisi ya Manispaa wanaweza kupata huduma hiyo.

Katika ngazi ya vitongoji viongozi wote wa kuchaguliwa wakiongozwa na mwenyekiti wa serikali za mitaa kazi yao itakuwa ya kuhamasisha huku watendaji wakihusika na ukusanyaji.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano na kuwataka wenye nyumba ambao nyumba zao hazijasajiliwa kufanya hivyo ili waepuke adhabu ya kulimbikiza kodi.

Pia Mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni Mhandisi Musa Natty pamoja na kuwataka watendaji watendaji kufanya kazi zao kwa uaminifu mkubwa aliwatahadharisha watakaoiba watachukuliwa hatua za kisheria.Aliseama viongoziwa kuchaguliwa(wakiwemo wenyeviti wa serikali za mitaa)kutokana na ukusanyaji wa kodi hizo za jengo watapata asilimia 7(7%).Imetolewa Na Manispaa Ya Kinondoni

No comments:

Post a Comment