Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 23, 2014

Misri yaiomba TZ iisaidie kurejeshewa uanachama AU



Serikali ya Misri imeiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iisaidie ili irejeshewe uanachama wake katika Umoja wa Afrika AU. 
Ombi hilo limetolewa na Nabil Fahmy, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Misri mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam Tanzania. 
Katika mazungumzo yake na Bernard Membe, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Nabil Fahmy amesema wanaoimba serikali ya Tanzania iisaidie Misri ili irejeshewe uanachama wake katika Umoja wa Afrika. 
Bernard Membe, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania amesema kuwa, atawasilisha ombi hilo la Misri kwa Rais Jakaya Kikwete. 
Misri ilisimamishwa uanachama katika Umoja wa Afrika tangu Julai mwaka jana baada ya Rais halali wa nchi hiyo Muhammad Mursi kuondolewa madarakani na jeshi. 
Hadi sasa nchi hiyo bado haijarejeshewa uanachama katika Umoja wa Afrika.

Chanzo: kiswahili.irib.ir

No comments:

Post a Comment