Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, February 12, 2014

MOURIHNO AIPINGA FA KWA KUTOMPA ADHABU YAYA TOURE

pelle-mou_5c0ff.jpg
Kocha wa timu ya Chelsea Jose Mourihno ameupinga umoja wa shirikisho la soka la uingereza (FA) kwa kutompa adhabu kiungo wa timu ya Manchester City, yaya toure ambaye aliyemchezea rafu mchezaji wa Norwich city ajulikanaye kama Ricky Van Wolfswinkel katika mchezo ambao ulioshuhudia timu hizo zikitoka sare (0-0), katika uwanja wa Carrow Road; Mourihno alisema kuwa mwamuzi ''Jonathan Moss'' alitakiwa kumpa adhabu kali kiungo huyo wa Manchester City na pia umoja wa shirikisho la uingereza ulitakiwa kumpa adhabu kali Yaya Toure kwani kumwachia huru ni kuchora picha mbaya katika soka la uingereza na kuwapa uhuru wachezaji kucheza rafu.

Mourihno alisema kuwa kwa mtindo huo wachezaji wengi watakuwa wanachezeana rafu na kuzidi kudharau sheria na kanuni za umoja huo wa FA; kocha huyo mwenye asili ya kireno amekuwa akiongea maneno mengi kuhusu timu ya Manchester City katika kipindi hiki kifupi hususan matumizi makubwa ya fedha ambayo yanafanywa na klabu ya Manchester City katika soka kinyume na utaratibu lakini kinachofuraisha ni kwamba kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekuwa mkimya na hawajahi kumjibu kocha huyo mwenye maneno mengi.
Chanzo, goal.com

No comments:

Post a Comment