Naibu Waziri
wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Nchemba hii leo asubuhi (Tar. 05/02/2014)
amekutana na Watendaji/Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Hazina Ndogo na Wahakiki Mali za Serikali Mkoani Mbeya kwa ajili ya
kufahamiana nao, pia kuzungumza nao kuhusu uboreshaji
wa ukusanyaji wa mapato nchini, msimamo wa Serikali kuhusu matumizi ya
mashine za EFD kwenye ulipaji kodi na pia uadilifu na ushirikiano katika
utumishi wa umma, hususani kwenye Wizara ya Fedha.
Akizungumza na watendaji hao, Naibu Waziri amesema Serikali imejipanga
na itaendelea kusimamia zoezi la kuhakikisha wafanyabiashara wanatumia
mashine za EFD ilikukusanya kodi halisi ya bidhaa/huduma wanazotoa kwa
wananchi: "Utumiaji wa mashine za EFD kwa wafanyabiashara unaboresha
kipato halisi cha bidhaa wanazoziuza, pia mashine zinasaidia kudhibiti
mianya ya ukwepaji wa kulipa kodi nchini."
Kwa
mkoa wa Mbeya wenye wafanyabiashara walipa kodi waliojiandikisha 32,647
kuna zaidi ya wafanyabiashara 297 walionunua mashine za EFD na zaidi ya
300 wameshaanza kulipa kwa awamu iliwaweze kupatiwa mashine hizo. Idadi
hii ya wanunuzi wa mashine za EFD imeongezeka kwa kasi mara baada ya
mgomo wa wafanyabiashara uliofanyika 1/10/2013 kupinga matumizi ya
mashine hizo.TRA kupitia mawakala wake wamekuwa wakitoa elimu ya
matumizi ya mashine hizo kwa wafanyabiashara na hatimaye uelewa umekuwa
mkubwa na sasa wengi wamejitokeza kununua mashine hizo.
Pia
Mhe. Nchemba amesisitiza ushirikiano na umoja kwenye utumishi wa Ofisi
za umma hususani hizi za ukusanyaji wa kodi nchini: "Haikubaliki kwa
mtendaji/mtumishi wa TRA na idara husika za mapato kufanya ubadhirifu wa
kodi za Watanzania wakati serikali inatumia nguvu kubwa kuhakikisha
kodi inakusanywa kwenye vyanzo vyote.Ni wajibu kwa kila mtumishi kufuata
sheria za nchi za utumishi ili kuondokana na adha atakayoipata pindi
ofisi yake ikibaini kuna watendaji wanaofanya ubadhirifu wa kodi za
Watanzania."
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu
Nchemba akiwasili Ofisi za Mamlaka ya Mapato TRA mkoani Mbeya hii leo
wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kutembelea Ofisi zote za TRA, Ofisi za
Hazina ndogo na kuzungumza na wafanyabiashara katika mikoa ya Njombe,
Ruvuma na sasa Mbeya.
Naibu Waziri wa Fedha (sera) Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Mbeya mapema hii leo.

No comments:
Post a Comment