Mwenyekiti wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba |
MWENYEKITI wa halimashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba amepokea
maombi ya kuhamasishwa mchezo wa masumbwi katika halimashahuri hiyo
baada ya mchezo huo kufutuka kwa kipindi hiki
Maombi hayo yaliyopelekwa na kamati ya kufufua mchezo wa masumbwi
Kisarawe ikiongozwa na Bondia Mbaruku heri, Kocha wa Kimataifa wa mchezo
wa ngumi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' pamoja na wadau wengine wa
masumbwi nchini Saidi Chaku na Masudi Bakari ambao wamepereka barua hiyo
kwa ajili ya kurudisha hamasa ya mchezo wa masumbwi
akizungumza
mara baada ya kusoma maombi yaliyopo katika barua hiyo alijibu kwa
kusema nimepokea kwa moyo mmoja maombi haya na ngumi zitapigwa kama
zamani nakumbuka mabondia wengi akiwemo Habibu Kinyogoli 'Masta'
ametokea hukuhuku Kisarawe na mkumbuke kuwa bondia wa ngumi za ridhaa
anaetamba kwa sasa na aliyetuwakilisha katika mashindano ya Olimpic
yaliyomalizika hivi karibuni Selemani Kidunda naye anatoka hapa hapa
katika wilaya ya Kisarawe hivyo tunaweza kuhakikisha ngumi zinarudia
enzi zake
na
naku aididi ngumi hizi zitapigwa katika viwanja vya wazi ili kila mtu
ashudie mchezo wa ngumi unavyorudi upya katika wilaya hii naomba wapenzi
mashabiki wa mchezo wa masumbwi wakae mkao wa kula siku ya April 26
ngumi zitapigwa katika uwanja wa bomani ili kila mtu ajionee mwenyewe
aliongeza
kwa kusema ataendelea kutafuta wafadhili ili walete hamasa ya mchezo wa
ngumi katika wilaya hiyo ambayo imejinyakulia umaarufu mkubwa mpaka
sasa kupitia mchezo wa ngumi nita akikisha tunanunua vifaa vya mchezo
ili vijana wapate kuendelea kushiriki mazoezi na atimae waje kurudia
enzi za Kinyogoli
nae
mkuu wa msafara wa kuhamasisha mchezo wa ngumi katika wilaya
hiyo, Mbaruku Heri amesema atakikisha siku hiyo analeta vijana wengi
wakali wanaotamba katika ulimwengu wa masumbwi kwa sasa kama vile
Ibrahimu Class 'King Class Mawe',Hamza Mchanjo,Thobias Adaut, Husein
Pendeza,Said Uwezo,Adamu Ngange,Ambokile Chusa,Georgr Dimoso,Twalibu
Mchanjo na wengine wengi wanaofanya vizuri katika ulimwengu wa masumbwi
kwa sasa
No comments:
Post a Comment