MWENYEKITI
wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewapa rungu wana-CCM akiwataka kuacha
kujifanya wanyonge dhidi ya vitendo vya fujo ambavyo hufanyiwa na
Chadema hasa nyakati za uchaguzi.
Rais Kikwete amesema hayo leo, wakati akiongoza kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma.
"Uchaguzi wa Kalenga ndiyo huo upo mbele yetu, hadi sasa hakuna tatizo
lililojitokeza kama Arumeru mambo yapo shwari kabisa, lakini tujue tu
kwamba pale tunaenda kushindana na watu (Chadema) ambao wao silaha yao
ya kwanza ni vujo.. ninaagiza sasa lazima wana CCM kukabiliana na fujo
zao. Unyonge basi.", alisema Rais Kikwete na kuongfeza;
"CCM kuendelea kujifanya wanyonge kila mara sasa basi. Haiwezekazi watu
wanafanya vujo hadi kuwatoboa watu macho ninyi nmanyongea tu, hili
haliwezekani. Tazama pale Ingunga mtu wenu alimwagiwa tindikali hadi
leo ana ulemavu wa kudumu kisa uchaguzi tu, aah haiwezekani kabisa",
alisema Rais Kikwete.
Mapema Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete alipongeza wana CCM na viongozi
wao katika Kata zote zilizofanya uchaguzi mdogo wa Udiwani na hatimaye
CCM kuibuka na ushindi wa Kata 23, Chadema ikiambulia tatu na NCCR
Mageuzi kimoja.
Hata hivyo Rais Kikwete alisema, licha ya CCM kuzoa kata nyingi kwenye
uchaguzi huo, viti vinne kwenda kwa upinzani bado ni doa hivyo lazima
CCM ihakikishe inazikomboa kata hizo nyakati za chaguzi zijazo.
"Ni kweli tumezoa kata nyingi, lakini kwa kuwa lengo letu CCM kila
wakati ni kushinda tu, hatua hiyo ya kuzikosa kata nne bado ni doa
lazima kuzikomboa kata hizo chaguzi zijazo", alisema, Rais Kikwete.
Pia alipongeza CCM, kwa ushindi iliopata kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo
la Kimbesamaki na kwamba CCM inaona fahari kulirejesha jimbo hilo
mikononi mwake, kwa kuwa ilikuwa imelazimika kumfuza mwakilishi wake wa
awali kwenye jimbo hilo kwa kuwa alikuwa msaliti aiyefaa kuendelea
kuwemo ndani ya Chama. CHANZO BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment