ISO 9001: 2008 CERTIFIED
TAARIFA KWA UMMA
Mamalaka
ya Mapato Tanzania inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania na
wafanyabiashara kwa ujumla Kuwa inasikitishwa na mgomo wa
wafanyabishara kwa kufunga maduka maeneo mbali mbali nchini.
Ifahamike
kuwa Matumizi ya mashine ya EFD ni jambo la kisheria na lilipitishwa
na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2011.
Pamoja
na sheria kupitishwa, viongozi wakuu wa nchi walikwisha litolea tamko
kwa nyakati tofauti kwa kuanzia na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake ya kufunga mwezi
wa Machi 2011.
Pia
Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohammed Gharib
Billal alikazia jambo hili tarehe 8 Mwezi November mwaka 2013.
Waziri
mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Mizengo Peter Pinda
alilitolea tamko pia Mwezi Desemba 2013 wakati akiahirisha Bunge kwa
kusisitiza msimamo wa serikali kwa utekelezaji wa kisheria wa matumizi
wa mashine za EFD.
Tarehe
29 Janauri 2014, Waziri wa Fedha Mhe Saada Mkuya Salum aliweka bayana
msimamo wa Serikali kwa kusisitiza kuwa Matumizi ya mashine za EFD ni
swala la kisheria na litaendelea kutekelezwa kwa mujibu wa sheria
akisisitiza kuwa muda wa mwisho wa nyongeza kwa wafanyabishara kununua
mashine ilikuwa ni Tarehe 31 Januari 2014 baada ya kuongeza muda mara
tatu kwa nyakati tofuati.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) pia kwa nyakati tofauti na maeneo tofuati
imelitolea tamko jambo hili na itaendelea kufanya hivyo.
Kwa masuala ya kiutendaji yaliyolalamikiwa yamefanyiwa kazi na yanaendelea kufanyiwa kazi ikiwemo utoaji wa Elimu kwa umma.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania inapenda kuwafahamisha wafanyabiashara na umma kwa
ujumla kuwa watu wanaolazimisha wafanyabishara wenzao kufunga maduka kwa
kuwatishia na kuwashurutisha wanavunja sheria kwa kusababisha uvunjifu
wa amani nchini na hivyo mkono wa sheria utawafikia. Pia imefahamika
kuwa baadhi ya watu wanaoshurutishwa kufunga biashara sio walengwa bali
hutumika kuhalalisha azma ya wale wenye nia mbaya
TRA
imekuwa ikipokea taarifa na maombi kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara
na wananchi wema wakiomba ulinzi ili wafungue maduka yao na kufanya
biashara maana ndio ajira yao na mahali pakujipatia riziki ya kila siku.
Ifahamike
kwamba wale wote wanaoshinikiza na kulazimisha wenzao kugoma wanavunja
sheria kwa kuwalazimishwa wafanyabiashara kugomea agizo halali la
kisheria hivyo kwa wale wote wanaotishiwa au kushurutiswa watoe taarifa
kwa kupiga simu namba zifuatazo 0786 800 000, 0713 800333, 0800 110016
au barua pepe info@tra.go.tz
“PAMOJA TUNAJENGA TAIFA LETU”
IMETOLEWA NA KAIMU KAMISHNA MKUU
No comments:
Post a Comment