Taarifa iliyotolewa na Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mara Claud Kanyorota imesema watu hao waliokamatwa wamekili kuhusika na matukio kadhaa ya mauaji ya Wanawake kutokana na imani za kishirikina.
Amesema kutokana na oparesheni inayoendeshwa na jeshi la polisi kutokana na mauaji hayo walifanikiwa kuwakamata watu hao na kutoa nyavu ambazo walikuwa wakizitumia baada ya kufanya matukio ya mauji ili wapate samaki ikiwa ni imani ya ushirikina.
Amesema oparesheni hiyo itakuwa ya kudumu kuhakikisha matukio ya mauji ya Wanawake yanayotokea wilayani Butiama na maeneo mengine ya mkoa wa Mara yanakomeshwa ili Wanawake waendelee kufanya shughuli zao za kiuchumi bila kuwa na hofo yoyote.
Katika tukio lingine,Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara amesema Mkuu
wa kituo cha Polisi Buhemba
wilayani Butiama na askari wenzake wamekamata bunduki aina ya SMG/SAR na
risasi 38 baada ya kufanya upekuzi kwenye nyumba ya Bhoke Kamau(37)
zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala la chakula baada ya kupata taarifa
kutoka kwa wananchi.
Watu
wengine waliokamatwa baada ya upekuzi huo ni Mgosi Silvester(34), Mlimi
Silvester na Juma Kabondo(52) wote wakiwa ni wakazi wa wilaya hiyo na
kwamba
watuhumiwa hao wanatarajia kufikishwa Mahakamani muda wowote.
BAADAE HABARI ZILIFIKIA BLOG HII NA KUDAI KUWA WATUHUMIWA HAO TAYARI WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUFUNGULIWA MADA KESI NAMBA 4 YA MWAKA 2014
No comments:
Post a Comment