Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi alisema viashiria vinavyosababisha mvua za masika mwaka huu ni kuwapo kwa joto la chini la wastani katika eneo la Bahari ya Atlantiki (Pwani ya Angola) ambalo linatarajiwa kuwapo kwa kipindi chote cha msimu.
Alisema mvua za masika zitanyesha katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka na zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Machi.
Alisema mvua hizo zinatarajiwa kuanza Kanda ya Ziwa Victoria katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu na zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza kwenye mikoa ya Geita na Kagera na kusambaa mikoa mingine katika wiki ya pili na inatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani.
Aidha, alisema katika Nyanda za Juu Kusini Magharibi yenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Katavi, mvua zinazoendelea kunyesha zinatarajia kuwa za wastani hadi juu ya wastani isipokuwa maeneo ya mikoa ya Njombe ambapo zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani.
Alisema maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za juu ya wastani kuna uwezekano wa milipuko ya magonjwa kama vile malaria, kipindupindu, kuhara damu na homa za matumbo.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment