OFM yamuokoa mtoto wa huyu.
Huu ni
zaidi ya unyama! Mama ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi huko
Tandika, Dar, almaarufu kwa jina la Mama Kumburu, anatuhumiwa kwa
unyanyasaji wa kijinsia wa mtoto wa miaka 10 kisha kutiwa mbaroni.
Baada
ya kupata malalamiko ya raia kuwa kuna mtoto anatumikishwa kazi za mtu
mzima, hivi karibuni Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) iliingia
mzigoni na kwenda kumwokoa mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la
pili wa shule ya msingi huko Temeke.
Awali,
OFM ilifika nyumbani kwa mama huyo maeneo hayo ya Tandika ili
kujiridhisha na tuhuma hizo ambapo ilijionea jinsi mama huyo
anavyomtumikisha na kumnyanyasa mtoto huyo.
Kwa
mujibu wa majirani, mtoto huyo ambaye yupo chini ya umri wa miaka 18,
huamshwa saa 11:00 alfajiri na kutakiwa kufanya kazi zote za ndani
(isipokuwa kupika) na kwenda kuchota maji kwa mkokoteni kila siku, tena
umbali mrefu huku ikidaiwa kuwa hufanya hivyo mara tatu au nne kwa siku
bila kula.
Mtoto huyo akichoteshwa maji.
Kama
hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa mara kwa mara mtoto huyo hupewa kipigo
kikali kwa makosa ya kawaida, kiasi cha majirani kukerwa na vitendo
hivyo na kumuomba mama huyo aache mara moja tabia hiyo lakini hakusikia.
Ilidaiwa
kwamba siku moja kabla ya kukamatwa kwa mwalimu huyo, mtoto huyo
alipokea vipigo mfululizo kisa alimsindikiza jirani yake aliyeomba aende
naye mahali.
Siku
ya tukio OFM ilimtafuta mtoto huyo ambapo ilimkuta akijiandaa kwenda
shule na kujionea jinsi alivyodhoofu na kujaa makovu mwilini.
Mama mtuhumiwa almaarufu kwa jina la Mama Kumburu (wa pili kutoka kushoto) akipelekwa polisi.
OFM
ilimfuatilia mtoto huyo hadi shule anayosoma na kujionea jinsi
maendeleo yake kimasomo yasivyoridhisha huku akijitenga na wenzake na
kuwa mtu mwenye wasiwasi na huzuni muda wote.
Majira
ya saa 11:00 jioni, OFM, ikiwa na polisi wa dawati la jinsia kutoka
Mbagala-Kizuiani ‘iliseti’ mitego yake kila kona na kupata taarifa kuwa
shangazi wa mtoto huyo ambaye ndiye anayedaiwa kuhusika na unyanyasaji
huo, alikuwa tayari amerejea kutoka kazini hivyo kwa muda huo mtoto huyo
angeanza kufanyishwa kazi ikiwemo kuchota maji jambo ambalo lilikuwa
kweli.
Haraka,
OFM ilimfuatilia mtoto huyo akiwa na tolori la maji lenye madumu manne
hadi bombani ambapo mwenyewe alisema aliambiwa na shangazi yake, arudie
kuchota maji mara nne, jambo ambalo lilikuwa kweli.
OFM ilimshuhudia mtoto huyo akijaza madumu ya maji na kulisukuma
tolori hilo kwa tabu huku kila aliyemuona akiishia kumsikitikia jambo
lililowalazimu OFM wamsaidie huku wakiongozana na polisi hao hadi
nyumbani kwao na kumkamata mama huyo.
Akionesha ubabe wake, mwanamama huyo awatolea maneno machafu OFM na
polisi waliokuwa eneo hilo na kudai kuwa yeye anafahamiana na watu
wakubwa na kamwe hawezi kwenda rumande.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Hata hivyo, baada ya kuona
mambo yanakuwa magumu, mama huyo alikubali kuelekea kituoni ambapo
alifunguliwa jalada la kesi namba MBL/RB/1827/2014- UNYANYASAJI huku
mtoto huyo akiwekwa chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii.
No comments:
Post a Comment