Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 9, 2014

Update: Jeshi la Polisi Lamkamata Jambazi Sugu aliyehusika na Mauaji ya watu 8 huko Tarime.

jeshi
Mkuu wa jeshi la polisi nchini  via Imma Matukio — Jambazi mkuu anayetuhumiwa kujihusisha na matukio ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyo tokea Wilayani Tarime kuanzia 26 hadi 28.01.2014 amekamatwa na jeshi la polisi jioni ya Tarehe 06.02.2014 mkoani Tanga.
 
Akisimulia kukamatwa kwa jambazi huyo Kamanda wa mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jioni ya Tarehe 06.02.2014 majira ya saa 1.30 na katika mahojiano ya awali ya jeshi la polisi mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na matukio ya mauaji ya kuanzia tarehe 26 hadi 28 na unyang’anyi wa kutumia silaha pamoja na mengine.
 
Kamugisha alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Bw. Chaerles Range Kichune, 38 maafuru kama Josephat Chacha ama Joseph Charles Chacha Msong’o mkazi wa Kenyamanyori kata ya Turwa Wilayani Tarime.
Aidha Kamugisha amesema kuwa mtuhumiwa alimtaja Marwa Keryoba Alex 30 – 38 mkazi wa Kijiji cha Kebeyo Sirari Wilayani kuwa wanashirikiana kufanya ujambazi na silaha ametunzia nyumbani kwake huko Musoma.
‘“Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifuatilia hadi nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo walimkuta na alipo waona maasikari polisi alijaribu kukimbia huku akiwa amebeba silaha aina ya (bunduki) SMG .Askari walipiga risasi hewani wakimtaka kujisalimisha lakini alikaidi na kuanza kuwarushia risasi na ndipo asikari waliendelea kurushiana risasi na hatimaye kumpiga risasi, marehemu alifia njiani akiwa anapelekwa hospitalini kwa matibabu,” alisema Kamugisha.
 
Kamugisha ameendelea kusimulia kuwa marehemu alikutwa akiwa na Bunduki anina ya SMG moja na iliyo futwa namba na kukatwa kitako na mtutu,magazine moja na risasi kumi katika upekuzi nyumbani kwake polisi wamefanikiwa kupata vitu kadhaa vikiwemo simu mbili za mkononi , CD 21 za picha mbalimbali deki moja,viatu pea mbili na tochi mbili na mpira wa baiskeli moja na bidha mbalimbali za dukani.
 
Pia Kamanda alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 1.45  Februari 7, 2014 katika Kijiji cha Nyabisare kata ya Bweri Mjini Musoma mkoani Mara ambapo marehemu ameuawa kutokana na taarifa zilizo tolewa na Bw Charles Chacha Kichune maafuru (kenonke) ambaye  amemtaja marehemu kuwa ni mshirika wake.
 
Kamugisha ameshukuru jeshi la polisi Mkoa wa Tanga kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi Tarime/Rorya kuhakikisha jambazi huyo anakamatwa.Pia amewataka wananchi kuwa watulivu na kuendelea kufanya shuguli zao kama kawaida wakati hatua zingine zinachukuliwa .
 
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano na yeyote atakaye toa taarifa ya jambazi kukamatwa atapewa zawadi ya Tsh milioni moja papo hapo

No comments:

Post a Comment