Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Thomas Kashillilah,
amewaambia waandishi wa habari kuwa Bunge Maalumu la Katiba
litazinduliwa rasmi Februari 26, 2014 huku kila mjumbe akilipwa posho ya
shilingi laki tatu na siyo shilingi laki saba kama ilivyochapishwa
katika baadhi ya vyombo vya habari.
“Sisi tumesikia kuwa Wabunge wa Bunge la Katiba wanalipwa 700,000 na wala hatujui hili limetoka wapi, kwanza mamlaka ya kuidhibisha posho ni la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hajaidhinisha Sh. 700,000.
Alisema
Wajumbe watalipwa posho ya kawaida ya Serikali ya siku (hakuitaja),
lakini alisema kutawakuwa na kodi maalumu ambayo itahusisha posho ya
kikao, usafiri, malipo kwa madereva na mengineyo. Hivyo posho ya kawaida
itakuwa Sh 80,000/=
“Kwa hiyo posho aliyoidhinisha ni posho inayolipwa sasa..kwa maana fedha ya kujikimu ni sawa sawa na viwango vingine, kwa maana posho ya kikao na posho ya usafiri imechanganywa kwa pamoja inalipwa kama ni posho ambayo ni ya kawaida ambayo ni Sh. 220,000.
“Jumla Mbunge wa Bunge Maalum akija Dodoma akiingia kwenye kikao atalipwa Sh. 300,000”
Kashilillah
alisema Bunge Maalumu litajumuisha wajumbe 629 ambao ni wabunge wote wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 357, wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi (BLW) 82 na wajumbe wa kuteuliwa kwa uwakilishi 201.
Alisema kuwa katika idadi hiyo,
punguza wajumbe sita wa Baraza la Wawakilishi ambao pia ni wajumbe wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjumbe wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa
uteuzi wa Rais wa Zanzibar, wabunge wawili waliofariki na nafasi mbili
za uteuzi wa Rais zilizo wazi, hivyo unapata wajumbe 629.
Amesema
Bunge hilo litaanza kwa mkutano wa maelekezo ya ukaaji na jiografia ya
ukumbi kesho asubuhi na tayari utekelezaji wa ratiba umeanza jana kwa
kusajili wajumbe --ambapo zaidi ya 120 walikwisha jisajili hadi kufikia
jana mchana-- kazi ambayo itaendelea leo.
Amesema
kesho saa 8 mchana, kutasomwa tangazo la kuitisha Bunge Maalumu,
uchaguzi wa Mwenyekiti wa Muda na kuandaa na kupitisha Kanuni za Bunge
hilo.
"Mwenyekiti wa muda atachaguliwa kwa utaratibu maalumu uliowekwa na Katibu wa Bunge la Muungano na wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambao utaratibu tutatoa leo. Mwenyekiti wa Muda atasimamia kuchaguliwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,"
alisema Dk Kashillilah.
Alisema Mwenyekiti wa Muda
atakayechaguliwa Februari 21, pia atasimamia kuandaliwa kwa Kanuni, na
baada ya kupatikana kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, ndipo
atateuliwa Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo kwa mujibu wa sheria
kwani yeye na mwenzake wa Zanzibar kwa sasa wanasimamia tu mchakato huo.
Alisema kabla ya Mwenyekiti na
Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kuanza kazi zao, kwanza
watasubiri Rais kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu, na ndipo Katibu wa
Bunge hilo, atakuja kumwapisha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti; na
Mwenyekiti kuwaapisha wajumbe wake.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Jumatano
na Alhamisi zitatumika kwa kikao cha kazi cha kuandaa Rasimu ya Kanuni
za Bunge Maalumu, wakati Ijumaa itakuwa siku ya kupitisha Azimio la
kuridhia Kanuni za Bunge Maalumu, uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti na kiapo cha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalumu (ingawa
hiyo siyo shughuli ya Bunge Maalumu).
Dk Kashillilah alisema Jumamosi,
itakuwa ni kiapo cha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu na
kufuatiwa na kiapo cha wajumbe wa Bunge Maalumu ambacho kitaendelea
hadi Jumapili.
Aidha, Jumatatu pia kutakuwa na
kiapo cha wajumbe saa 4 asubuhi na kuunda Kamati za Bunge Maalumu, kabla
ya ufunguzi rasmi wa Bunge utakaofanywa na Rais Jakaya Kikwete, saa 10
jioni.
Alisema pia kuwa uwasilishwaji wa
Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu itakuwa ni Jumanne na Jumatano ya
Februari 26, mjadala wa kupitisha Rasimu ya Katiba utaanza hadi Aprili
30, mwaka huu.
“Baada ya uzinduzi huo kufanywa ndiyo Rasimu ya Katiba itawasilishwa kwa mpangilio tuliouanisha katika ratiba ambayo tutakuwa tumewapa... kwa hiyo baada ya pale Rasimu ikiwasilishwa na kanuni zitakuwa zimeainisha ni kwa utaratibu gani Rasimu hiyo kabla ya kuwasilishwa itajadiliwa hatua kwa hatua mpaka mwisho, ambapo sasa itakuwa imepatikana Katiba inayopendekezwa ili iende kwa wananchi kwa ajili ya kupata ridhaa,”
alisema Dk. Kashilila.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Bunge
Maalumu litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha masharti ya Katiba
inayopendekezwa na kutunga masharti ya Mpito na masharti yatokanayo kama
Bunge Maalumu litakavyoona inafaa.
Ili Katiba inayopendekezwa ipitishwe
katika Bunge Maalumu la Katiba, itahitajika kuungwa mkono kwa wingi wa
theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge Maalumu kutoka Tanzania
Bara na theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Tanzania Zanzibar.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko
ya Katiba, muda ambao Bunge Maalumu litajadili Rasimu ya Katiba
hautazidi siku 70 kuanzia tarehe ambayo Bunge Maalumu lilipoitishwa,
hivyo uhai wa Bunge hili unatarajiwa kukoma Aprili 30, mwaka huu, lakini
unaweza kuongezwa kwa mashauriano kati ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu
na Makamu wake kwa ridhaa ya Rais kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar.
UKARABATI ULIOGHARIMU BILIONI Sh8.2/=
Akizungumzia
gharama za ukarabati wa jengo na miundombinu mingine, Dk Kashillilah
alisema ni Sh bilioni 8.2, ambazo zote zimetoka katika Bajeti ya
Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/14 ambayo ilishapitishwa na Bunge
ikiwamo posho za wajumbe ambazo ni Sh 300,000 kwa siku kwa mjumbe.
"Fedha zote hizo zilikuwapo katika Bajeti ya Serikali iliyopitishwa Juni mwaka jana, kwa hiyo siyo suala geni. Na zimetumika katika ukarabati wa jengo la ukumbi, vifaa vikiwamo viti 678 ambavyo gharama yake ni dola za Marekani milioni moja,"
“Haya yote mliyoyaona yamefanyika hapa ni mambo ya kawaida ambayo yalikuwa kwenye bajeti la Bunge la Muungano wa Tanzania... si mambo mapya, yalikuwa tu yapo kwenye mchakato, sasa yote yamefanyika kwa wakati mmojaalifafanua Katibu wa Bunge.
No comments:
Post a Comment