Twiga Stars wanaotarajiwa kuwapa raha watanzania kesho |
WAKATI Zambia (Shepolopolo) imewasili leo
mchana (Februari 27 mwaka huu), Twiga Stars imesema mazoezi yamewaingia
barabara tayari kwa mechi dhidi ya Wazambia hao itakayochezwa kesho
(Februari 28 mwaka huu). Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya
michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itafanyika Uwanja wa Azam Complex
uliopo Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni, na hakutakuwa na
kiingilio. Wakizungumzia mechi hiyo, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian
Kaijage na nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili wamesema kikosi chao
kimewiva kwa ajili ya mpambano huo baada ya kufanyia kazi upungufu
uliojitokeza katika mechi ya kwanza.
Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza
iliyochezwa Februari 14 mwaka huu jijini Lusaka kwa mabao 2-1, na
inahitaji ushindi ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo
fainali zake zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini Namibia.
Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia
katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv itacheza
raundi ya mwisho na Zimbabwe.
Msafara wa Shepolopolo una watu 26 ambapo
wachezaji ni Anita Mulenga, Annie Kibanji, Carol Howes, Debora Chisanga,
Emelda Musonda, Esther Mukwasa, Grace Zulu, Hazel Nali, Hellen Mubanga,
Lweendo Chisamu, Meya Banda, Mirriam Katamanda, Misozi Zulu, Mupopo
Kabange, Noria Sosala, Rachel Lungu na Susan Banda.
Viongozi ni Maclean Daka, Charles Bwale,
Kaluba Kangwa, Enala Phiri, Cornelia Chazura, James Nyimbili, Besa
Chibwe, Dorothy Sampa na Kabungo Katongo.
No comments:
Post a Comment