Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa kwanza kutoka kushoto
akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Maria Stopes nchini Tanzania
Ulla Muller aliyekaa katikati ambaye alimtembelea Waziri wa Mambo wa
Ndani ya Nchi ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha baada ya
Rais Jakaya Kikwete kumteua Waziri Chikawe hivi karibuni kuiongoza
Wizara hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa kwanza kutoka kushoto
akifafanua jambo kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi mbele ya Mkurugenzi Mkazi wa Maria Stopes
nchini Tanzania Ulla Muller aliyekaa katikati ambaye alimtembelea Waziri
Chikawe ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha baada ya Waziri
Chikawe kuteuliwa hivi karibuni kuiongoza Wizara hiyo, Kulia ni Michael
Holscher Mkurugenzi wa Kimataifa wa Program za Maria Stopes ambaye
aliambatana na Mkurugenzi Muller.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa pili kutoka kushoto
akisikiliza utambulisho wa Balozi wa China Nchini Tanzania wa tatu
kutoka kushoto LU Youqing baada ya Balozi huyo kumtembelea Waziri
Chikawe Ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha , Utambulisho huo
ulitolewa na Mjumbe kutoka Ubalozi wa China hapa nchini wa kwanza
kutoka kushoto. Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa kwanza kutoka kushoto
akisikiliza jambo kutoka kwa Balozi wa China Nchini Tanzania wa tatu
kutoka kushoto LU Youqing baada ya Balozi huyo kumtembelea Waziri
Chikawe Ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha.Hivi karibuni Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Alimteuwa Waziri Mathias Chikawe Kuiongoza Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment