skip to main |
skip to sidebar
YANGA YAWASILI COMORO,WAANZA MAZOEZI
Wachezaji wa Young Africans wakifanya mazoezi leo jioni katika uwanja mdogo uliopo katika Hotel ya Retaj -Moroni
Kikosi cha Young Africans
kimewasili tayari kimewasili salama katika Visiwa vya Comoro majira ya
saa 6 kamili mchana kwa shirika la ndege la Precison Air na kupokelewa
na wenyeji wao kisha moja kwa moja kuelekea katika hotel ya Retaj Moroni
ambapo ndipo msafara wa watu 30 ulipofikia.
Mara baada ya kuwasili
Uwanja wa ndege mvua kubwa iliyoambatana na upepo ilinyesha hali
iliyopelekea pia timu kuchelewa kutoka Uwanja wa ndege kuelekea Hoteli
ambapo timu ilifika Ratej hoteli majira ya saa 9 mchana.
Kocha
mkuu wa Young Africans jioni amekiongoza kikosi chake kufanya mazoezi
mepesi katika uwanja mdogo uliopo hotelini kutokana na mvua na umbali wa
kwenda mji wa Mitsamihuli ambapo ndipo kuna uwanja utakaotumika kwa
ajili ya mchezo siku ya jumamosi.
Hali ya
wachezaji wote ni safi na hakuna majeruhi hata mmoja kuelekea kwenye
mchezo huo, ambapo kesho asubuhi majira ya saa 4 kikosi cha Young
Africans kitafanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa Said Mohamed Cheick
Mitsamihuli kwa ajili ya mchezo utakaofanyika siku ya jumamosi majira ya
9 kamili kwa saa za Visiwa vya Comoro.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
No comments:
Post a Comment