Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, March 20, 2014

AUAWA KWA KUCHOMA KISU NA MUME MWENZIE, KISA WIVU WA KIMAPENZI MAKETE(IRINGA)



Mkazi wa kijiji cha Mago kata ya Lupalilo wilayani Makete mkoa wa Njombe Bw. Frenk Sanga (35) ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kushoto ambao ndipo moyo ulipo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 17 mwaka huu majira ya saa 7 usiku, ambapo mtuhumiwa aitwaye Yohana Sanga alimchoma kisu kifuani baada ya kumfumania akiwa na mpenzi wake(hawara) aliyetambulika kwa jina la Matilda Sanga ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho cha Mago
Imeelezwa kuwa siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Bi. Matilda, waliongozana usiku hadi nyumbani kwa mwanamke huyo kwa ajili ya kulala pamoja, na ndipo mtuhumiwa ambaye ni Yohana, ambaye inadaiwa alikuwa akifuatilia nyendo zao aliwavamia nyumbani kwa mwanamke huyo na kumchoma kisu kifuani marehemu hadi akapoteza maisha
Baada ya mtuhumiwa kutenda mauaji hayo katika nyumba ya huyo hawara yake alichomoa kisu hicho na kumshikisha marehemu mkononi, kwa lengo la kupoteza ushaidi ili ionekane kuwa alijiua mwenyewe
Akizungumzia tukio hilo Afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Makete ambaye pia ni Kaimu OCD wilaya ya Makete, Mrakibu wa polisi Gosbert Komba amesema wao kama jeshi la polisi walipewa taarifa 
na Bw. Emannuel Sanga (25) ambaye aligundua kuuawa kwa marehemu Frenk na wao kama polisi walifuka eneo la tukio na kuthibitisha mauaji hayo
Bw. Komba amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo amekimbia mara baada ya tukio na jeshi hilo linamtafuta na kutoa wito kwa wananchi kwa kuwa mtuhumiwa anafahamika watoe taarifa polisi endapo watamuona ili atiwe mbaroni
Amesema kwa sasa wanamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo, na katika mahojiano na jeshi hilo mwanamke huyo amesema alishaachana na Yohana ambaye ni mtuhumiwa aliyetenda mauaji hayo na kwa sasa mapenzi yake yalikuwa kwa marehemu Frenk
"Kwa kawaida huyu mwanamke aligonganisha magari (aligonganisha wapenzi), na sisi kama polisi tunatoa wito kwa hawa dada zetu au wanawake, kuwa na mpenzi mmoja, lakini pia watu wasijichukulie sheria mkononi" alisema Komba
Wakizungumza na mwandishi wetu baada ya kumzika marehemu hii leo, baadhi ya wananchi ambao wametaka majina yao yahifadhiwe wamesema, mwanamke huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wote wawili kwa wakati mmoja jambo lililosababisha kifo Frenk
Wamesema licha ya mauaji hayo kutokea usiku na mwanamke huyo kushuhudia, hakupiga kelele za kuomba msaada wala kutoa taarifa kwa majirani bali alikaa kimya hadi wapita njia walipogundua mauaji hayo jana jambo linalowapa wasiwasi wananchi hao kuwa huwenda mwanamke huyo anafahamu kilichokuwa kikiendelea.

No comments:

Post a Comment