
Balozi
Mdogo wa Ethiopia Mhe. Yibeltal A. Alemu akikaribishwa na Balozi Mdogo
wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga alipomtembelea ofisini kwake leo
mjini Dubai.

Balozi Mdogo wa Ethiopia Mhe. Yibeltal A. Alemu na Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga katika mazungumzo.
Katika
mazungumzo yao wanadiplomasia hao walipata fursa ya kuzungumzia njia
muafaka na mbali mbali za kufanya kazi kwa karibu ili kuhakikisha
wanavutia utalii na uwekezaji katika nchi zao hasa kwa kuwavutia
wawekezaji kutoka wakubwa waliopo Dubai.
Mhe.
Mjenga alimuomba Mhe. Yibeltal kubadilishana uzoefu wa Ethiopia katika
kuvutia wawekezaji kutoka Dubai katika sekta ya kilimo. Alimuomba kuwa
Maafisa wa Biashara kutoka Balozi zote mbili wakutane ili kubadilishana
uzoefu huo ili Tanzania nayo iweze kuchukua mkondo huo kuwavutia
wawejezaji kwenye kilimo
No comments:
Post a Comment