Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Absalom Bohella (Kuliai) akizungumza na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake kukagua kukagua mirdai ya maendeleo Bandari hapo. Kutoka kushoto ni viongozi wa Timu hiyo, Prof. Longinus Rutasitara (Wakwanza Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Katikati).
Afisa Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Kushoto) akitoa maelezo ya uendelezaji wa maeneo ya Bandari hiyo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara Bandarini hapo.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea eneo la Bandari ya Mtwara ambapo panapotarajiwa kuongezwa magati
Afisa Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Wambele Kushoto) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango eneo jipya (halionekani) ambalo Bandari hiyo imeliongeza ili kuboresha ufanisi bandarini hapo.
Shehena
ya korosho ikiendelea kupakiwa katika makontena tayari kusafirishwa.
Afisa
Miradi Mwandamizi wa Bandari ya Mtwara, Bw. Norbert Kalebwe (Wambele Kushoto)
akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango eneo jipya (halionekani) ambalo Bandari hiyo imeliongeza ili kuboresha
ufanisi bandarini hapo.
Picha na Saidi
Mkabakuli
Ujenzi wa eneo la kuhifadhia saruji ukiendelea
Na
Saidi Mkabakuli
Mamlaka ya Bandari Tanzania, kupitia Bandari yake ya
Mtwara inajidhatiti katika kuiboresha ili kuiongezea uwezo wa kuhudumia mizigo
iingiayo na itokayo mkoani humo kupitia bandari hiyo kufuatia kuongezeka kwa
shughuli za biashara mkoani Mtwara.
Akizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Absalom Bohella amesema kwamba hatua hii
inachagizwa na mkakati wa kukabiliana na
kasi ya maendeleo ya ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na
biashara za huduma mkoani Mtwara.
Aliongeza kuwa mkakati huu unajumuisha upanuzi wa eneo la
bandari hiyo kutoka hekta 70 zilizokuwa zikimilikiwa na Bandari tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1950 hadi kufikia hekta zaidi ya 2600 pamoja na upanuzi
wa magati manne ya kuhudumia meli bandari hapo.
“Upanuzi huu utaongeza kasi yetu ya kuhudumia mizigo toka
tani za ujazo 270 za sasa hadi kufikia tani za ujazo 400 kwa mwaka hii
itatuongezea ufanisi katika kuhudumia watumiaji wa Bandari yetu, hasa kufuatia
kugundulika kwa gesi mkoani Mtwara,” alisema Bw. Bohella.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Katibu Mtendaji
(Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi
Florence Mwanri ambaye ni mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi hiyo
alisema kuwa kuna haja ya dhati ya kuwekeza katika Bandari hiyo ili kukabiliana
na kasi ya maendeleo ya mkoa wa Mtwara kufuatia wawekezaji wengi kuendelea
kumiminika na kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizomo mkoani humo.
“Bandari
ya Mtwara ina fursa za nyingi za kuhudumia wafanyabiashara wa ndani na nje ya
nchi, hasa katika kipindi hiki cha uchumi wa gesi mkoani Mtwara, hivyo
uendelezaji wa upanuzi wa bandari hii ni suala la kimkakati,” alisema Bibi
Mwanri.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 -
2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha
kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji
(bandari, reli, barabara na usafiri wa anga), maji (safi, taka na ya uzalishaji)
na TEHAMA.
Serikali
imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za
ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga
watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano
unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa
ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa
ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.
Lengo
la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi
ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment