Daktari
mmoja wa Hispania amedai kukutana na mgonjwa wa kwanza wa
‘WhatsAppitis’, tatizo lililotokana na kuchat kwa WhatsApp kwa muda
mrefu.
Mgonjwa huyo ambaye hakutajwa jina amedai kupata maumivu katika vifundo vya mkono alipoamka asubuhi.
Baada
ya madaktari kumfanyia uchunguzi mgonjwa huyo, walidai kuwa wamegundua
tatizo lake limetokana na kuchat kwa masaa sita kwa simu yake kwa
kutumia whatsApp.
Dokta
Inés Fernandez-Guerrero, wa Granada’s General University hospital
amesema kuwa mgonjwa huyo mwenye miaka 34 aliyekuwa na ujauzito wa wiki
27, alianza kusikia maumivu makali katika vifundo vyote vya mikono baada
ya kuamka asubuhi.
Baada
ya uchunguzi waligundua kuwa mgonjwa huyo hakuwa na historia ya
‘trauma’ na hakuwa ameshiriki katika shughuli yoyote ya kuchosha mwili
kupita kiasi katika siku zilizopita, lakini baada ya kuzungumza naye
tatizo likajiweka wazi.
Dokta
huyo alidai kuwa mgonjwa huyo alitumia simu yake yenye uzito wa g 130
kujibu messages za Whatsapp kwa masaa sita mfululizo.
Mgonjwa huyo alipewa dawa za kupunguza maumivu na kuzuiwa kutumia simu yake.
Madaktari
hao wamesema kuwa tatizo kama hilo ni jipya katika matatizo ya hi-tech,
na kuwashauri watumiaji wa App za kuchat kama WhatsApp, Viber na
zingine kuwa makini wanapochat kwa muda mrefu katika simu zao.
SOURCE: MAIL ONLINE
No comments:
Post a Comment