Jose Mourinho: Amesema Sir Alex Ferguson hastahili kulaumiwa
Kocha
wa Chelsea Jose Mourinho amewashangaa mashabiki wa Manchester United
wanaomlaumu Sir Alex Ferguson kutokana na matokeo mabaya wanayoyapata
msimu huu.
David
Moyes ndio ameanza changamoto ya kuiongoza Man United kwa msimu wa
kwanza, lakini baadhi ya mashabiki wanamnyoshea vidole Ferguson ambaye
alimteua kocha huyo kuwa mrithi wake.
“Watu wengi wanamuongelea Sir Alex. Aliwafanya Man United kuwa hatari”. Alisema Mourinho.
“Aliamua kustaafu. Mtu anapoamua kustaafu, hususani mtu kama yeye, anastahili kustaafu. Anatakiwa kufurahia maisha yake”.
“Sasa
anawajibika kwa lipi?, Man United wanapoteza mechi, huo ni wajibu
wake?, Man United kufanya vibaya ligi kuu ni tatizo lake?”.
“Rooney kukosa bao ni tatizo lake?, De Gea kufanya makosa ni kosa lake?”
No comments:
Post a Comment